Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pochettino mguu mmoja nje Marekani

POCHETINO Pict

Muktasari:

  • Mkataba wa Pochettino na Marekani unafikia tamati katika kipindi hiki cha Fainali za Kombe la Dunia na mabosi wa shirikisho la soka nchi hiyo wameonyesha utayari wa kumpa mkataba mpya lakini mwenyewe anaonekana ameshaamua vinginevyo.

LOS ANGELES, MAREKANI: BAADA ya kuiongoza Marekani kufika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026, Mauricio Pochettino anajiandaa kuachana na timu hiyo na kujiunga na mojawapo ya klabu za Ulaya.

Inaripotiwa kwamba licha ya Shirikisho la Soka Marekani kuonyesha nia ya kuendelea na Kocha huyo raia wa Argentina, Pochettino ameonyesha kuhitaji changamoto mpya jambo linaloilazimisha Marekani kuanza kusaka mkataba wake.

Mkataba wa Pochettino na Marekani unafikia tamati katika kipindi hiki cha Fainali za Kombe la Dunia na mabosi wa shirikisho la soka nchi hiyo wameonyesha utayari wa kumpa mkataba mpya lakini mwenyewe anaonekana ameshaamua vinginevyo.

AC Milan inayoshiriki Ligi Kuu Italia ‘Serie A’ inatajwa kuwa klabu ambayo inawania kwa udi na uvumba saini ya kocha huyo huku pia akiwa na ofa kutoka kwa baadhi ya klabu zinazoshiriki Ligi Kuu England.

Baada ya timu ya taifa ya Marekani kupoteza mechi dhidi ya Ubelgiji, Pochettino alikataa kujibu maswali kuhusu mustakabali wake.

“Huu si wakati wa kuzungumzia jambo hilo.Kwa sasa hakuna muda maalumu uliowekwa wa kufanya uamuzi,” amesema.