Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trump kushuhudia fainali ya Kombe la Dunia 2026

TRUMP Pict

Muktasari:

  • Rais wa FIFA, Gianni Infantino, tayari amethibitisha Trump atakuwa sehemu ya sherehe za kukabidhi kombe kwa mabingwa wapya mara baada ya mchezo kumalizika.

WASHINGTON, MAREKANI: IKULU ya Marekani (White House) imethibitisha Rais Donald Trump atahudhuria fainali ya Kombe la Dunia 2026 kati ya Argentina na Hispania itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa New York/New Jersey.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Trump kuhudhuria mechi ya mashindano hayo, licha ya kuonekana mara kadhaa akionyesha kuunga mkono soka na kushiriki maandalizi ya Kombe la Dunia linalofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino, tayari amethibitisha Trump atakuwa sehemu ya sherehe za kukabidhi kombe kwa mabingwa wapya mara baada ya mchezo kumalizika.

Hatua hiyo inaendeleza utamaduni wa viongozi wakuu wa nchi zinazokuwa wenyeji wa Kombe la Dunia kuhudhuria fainali.

Mwaka 2022, Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, alishiriki hafla ya kukabidhi kombe baada ya Argentina kutwaa ubingwa, huku mwaka 2018 Rais wa Urusi, Vladimir Putin, akihudhuria sherehe za kutawazwa kwa Ufaransa mjini Moscow.

Trump si mgeni katika hafla za FIFA. Mwaka jana alikabidhi Chelsea taji la Kombe la Dunia la Klabu, ingawa alizua mjadala baada ya kubaki jukwaani wakati wachezaji walipokuwa wakiinua kombe.

Baadaye kiungo Cole Palmer alikiri kuwa kitendo hicho kiliwashangaza wachezaji wa Chelsea.

Rais huyo pia ana uhusiano wa karibu na Infantino, ambaye alimkabidhi Tuzo ya Amani ya FIFA mwezi Desemba 2025.

Kabla ya fainali, Trump anatarajiwa kuhudhuria hafla maalumu ya FIFA itakayofanyika Trump Tower mjini New York kabla ya kuelekea uwanjani kushuhudia pambano la kusaka ubingwa kati ya Argentina na Hispania.