Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Szoboszlai atoa darasa la faulo

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hungary ambaye ni maarufu kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu, alionekana akimpa Elliott maelekezo ya namna ya kupiga mpira kwa usahihi na nguvu, huku video ya tukio hilo ikisambaa na kupata pongezi nyingi.

LIVERPOOL, ENGLAND: KIUNGO nyota wa Liverpool, Dominik Szoboszlai amemuonyesha mchezaji mwenzake Harvey Elliott jinsi ya kupiga mpira wa adhabu (free-kick) kwa ustadi wa hali ya juu, na matokeo yake yamewavutia mashabiki wengi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hungary ambaye ni maarufu kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu, alionekana akimpa Elliott maelekezo ya namna ya kupiga mpira kwa usahihi na nguvu, huku video ya tukio hilo ikisambaa na kupata pongezi nyingi.

Szoboszlai alifunga mabao 13 katika msimu mgumu wa 2025/26 yakiwemo mengi ya kuvutia yaliyotokana na mipira ya adhabu. Pia alitoa asisti 12 katika mechi 53 alizoichezea Liverpool, huku akifikisha mechi 100 akiwa na klabu hiyo.

Kiungo huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji muhimu walioisaidia Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England chini ya kocha Arne Slot katika msimu wa 2024/25.

Pia, alionekana kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa timu hiyo katika msimu uliopita kutokana na kiwango chake cha juu.

Na sasa Liverpool inatarajia Szoboszlai ataendelea kuwa na mchango mkubwa chini ya kocha mpya, Andoni Iraola, huku akiendelea kuwa mmoja wa viongozi kiufundi ndani ya kikosi na mfano kwa wachezaji wenzake, akiwemo Elliott.