Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Super Computer: Arsenal bingwa Ulaya 2026/27

BINGWA Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa ubashiri wa kompyuta maalumu ya Opta, Arsenal ina nafasi ya asilimia 20.9 ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imepewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, huku mabingwa watetezi Paris Saint-Germain (PSG) wakishuka hadi nafasi ya tano katika orodha ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba taji hilo.

Kwa mujibu wa ubashiri wa kompyuta maalumu ya Opta, Arsenal ina nafasi ya asilimia 20.9 ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu.

Ubashiri huo umefanywa baada ya kompyuta hiyo kufanya majaribio 10,000 ya msimu wa Ligi ya Mabingwa ili kubaini timu yenye uwezekano mkubwa wa kufika mbali zaidi.

Arsenal, ambayo msimu uliopita ilimaliza ikiwa mshindi wa pili, imepewa pia nafasi ya asilimia 34.8 ya kufika fainali na asilimia 50 ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Kikosi cha Mikel Arteta kilifika fainali kwa mara ya pili katika historia yake msimu uliopita, baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 2006.

Bayern Munich imeorodheshwa nafasi ya pili ikiwa na nafasi ya asilimia 19.4 ya kutwaa ubingwa huo, huku ikilenga kubeba taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2020.

BING 01

Manchester City inashika nafasi ya tatu kwa asilimia 12.3, ikifuatiwa na Barcelona yenye asilimia 8.2.

Barcelona, ambayo ilitwaa taji hilo mara ya mwisho mwaka 2015 kwa mara yake ya tano, imefika hatua ya nusu fainali mara mbili tangu wakati huo, mwaka 2019 na 2025.

PSG, ambayo ilitwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga Arsenal kwa penalti katika fainali ya Budapest kufuatia sare ya 1-1, imepewa nafasi ya asilimia 7.1 ya kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Hata hivyo, mabingwa hao wa Ufaransa wameanza msimu kwa kusuasua, wakipoteza dhidi ya Lens katika Super Cup ya Ufaransa, kabla ya kutoka sare na Rennes na Lille kwenye Ligue 1 na baadaye kufungwa 2-1 na Monaco mwishoni mwa wiki.

Liverpool ipo nafasi ya sita kwa asilimia 6.1, huku Real Madrid ikiwa nafasi ya saba kwa asilimia 4.4.

BING 02

Manchester United, ambayo inarejea kwenye mashindano hayo, imepewa nafasi ya asilimia 3.8 ya kutwaa ubingwa.

Orodha ya timu 10 zinazopewa nafasi kubwa zaidi inakamilishwa na Inter Milan, iliyomaliza ikiwa mshindi wa pili mwaka 2025, pamoja na Aston Villa, mabingwa wa Europa Ligi.

Kwa upande mwingine, PSG ilifikia hatua ya kihistoria msimu uliopita kwa kuwa timu ya pili baada ya Real Madrid kushinda Ligi ya Mabingwa mara mbili mfululizo katika enzi ya sasa ya mashindano hayo.