Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzanite Queens kujiuliza upya kwa England leo

TANZANITE Pict

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha kocha Bakari Shime wanakibarua kizito leo dhidi ya England  inayoshika nafasi ya tatu kwenye viwango vya ubora duniani, huku Tanzania ikiwa nafasi ya 122 kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

BAADA ya timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite Queens kuanza vibaya katika mechi yake ya kwanza ya Kundi B dhidi ya Brazil kwa kupokea kichapo cha mabao 4-1, sasa leo inashuka tena Uwanja wa Miejski saa 1:00 usiku kuikabili England.

Kikosi hicho cha kocha Bakari Shime wanakibarua kizito leo dhidi ya England  inayoshika nafasi ya tatu kwenye viwango vya ubora duniani, huku Tanzania ikiwa nafasi ya 122 kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Hivyo kuna umbali mkubwa wa viwango vya timu hizo mbili, lakini Tanzania ili ifanye vizuri kwenye mechi hiyo inahitaji kuingia uwanjani ikiwa na mpango tofauti, hasa kwenye namna ya kudhibiti kasi ya mpinzani, kuimarisha safu ya ulinzi na kutumia vizuri nafasi chache zitakazopatikana.

England yenyewe ilianza kampeni kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Canada, hivyo nayo inaingia kwenye mchezo huu ikitafuta ushindi wake wa kwanza. Rachel Maltby aliisawazishia England kwa penalti ya dakika ya 90, matokeo yaliyoiweka timu hiyo kwenye pointi moja pamoja na Canada.

Hilo linaifanya mechi ya Tanzania kuwa muhimu zaidi, kwa sababu ushindi wa timu yoyote unaweza kubadili kabisa sura ya Kundi B. Kwa Tanzania, kupata angalau pointi moja kutakuwa hatua muhimu kabla ya mchezo wa mwisho dhidi ya Canada.

TANZA 01

NAFASI

Kwanza, Tanzania inapaswa kupunguza nafasi kati ya safu zake. Dhidi ya Brazil, ilionekana kupata wakati mgumu pale mpinzani alipoongeza kasi na kuanza kutumia maeneo ya pembeni pamoja na nafasi zilizokuwa katikati. Pili, kiungo kinapaswa kuwa na nidhamu zaidi. England ina kikosi chenye wachezaji wenye uwezo wa kubadilisha kasi ya mchezo na kutumia mpira kwa utulivu. Tanzania ikipoteza mpira kirahisi katikati, inaweza kujikuta ikitumia muda mwingi kujilinda.

Tatu, mabeki wanapaswa kuwa makini kwenye mipira ya nyuma yao. Badala ya kusubiri England ifike kwenye eneo la hatari, Tanzania inahitaji kuzuia mashambulizi mapema na kuhakikisha inacheza kwa umoja kama timu.

TANZA 02

Lakini pia Tanzania inapaswa kutumia kasi ya Winfrida na washambuliaji wengine. Bao lake dhidi ya Brazil limeonyesha kuwa timu inaweza kupata nafasi za kufunga inapokuwa jasiri kwenda mbele.

Hivyo, si busara kutumia mchezo wote kujilinda unapokutana na timu kama England ambayo inakuja mara kwa mara kwa mpinzani.

England pia si timu isiyoweza kufungika. Sare yake dhidi ya Canada imeonyesha kuwa Tanzania inaweza kupata nafasi ikiwa itaingia kwenye mchezo ikiwa na ujasiri na mpangilio sahihi. Zaidi ya hapo, England yenyewe imesema inalenga kujipanga upya baada ya mchezo wa kwanza na kuangalia kwa karibu namna ya kuikabili Tanzania.

TANZA 03

Huu si mchezo wa kuingia uwanjani kwa hofu. Ni mchezo wa Tanzania kuonyesha kwamba kufuzu kwake kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia U-20 hakukuwa kwa bahati.

Tanzania inahitaji utulivu, nidhamu, ujasiri na matumizi mazuri ya nafasi ili kugeuza mchezo huo kuwa mwanzo mpya baada ya kipigo cha Brazil.

Winifrida amesema: “Hii sio mwisho. Tutaendelea kupambana, michezo yetu bado ipo miwili. Tutaendelea kupambana michezo inayokuja tuweze kupata pointi.

“Kila mmoja hapo atamsikiliza mwalimu kwenye nafasi yake anamwelekezaje. Pia tutakuja kiukubwa kuja kucheza mchezo wetu mechi na England.”

Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya wasichana ya Tanzania U20 kufuzu kucheza kwa fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake.