Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa aliyezimia uwanjani afariki

KIFO Pict

Muktasari:

  • Taarifa iliyotolewa na klabu ya Tenerife ilithibitisha kuwa mshambuliaji huyo alilazwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Nuestra Senora de Candelaria, huku hali yake ikielezwa kuwa ilitengemaa licha ya ukubwa wa tatizo alilolipata, lakini jana alitangazwa kufariki dunia.

TENERIFE, HISPANIA: MSHAMBULIAJI  wa CD Tenerife, Jesus de Miguel, amefariki dunia baada kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kufuati tukio la kutisha lililotokana na kugongana vibaya na kipa wa Andorra, Jesus Owono, katika mchezo wa Ligi Daraja la Pili Hispania uliofanyika Jumatatu iliyopita.

De Miguel, mwenye umri wa miaka 30, alizimia uwanjani dakika za nyongeza za kipindi cha pili, hali iliyosababisha mwamuzi kusitisha mchezo huo ukiwa sare ya mabao 2-2.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Tenerife ilithibitisha kuwa mshambuliaji huyo alilazwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Nuestra Senora de Candelaria, huku hali yake ikielezwa kuwa ilitengemaa licha ya ukubwa wa tatizo alilolipata, lakini jana alitangazwa kufariki dunia.

KIF 01

Hata hivyo klabu hiyo ilisema jana usiku kupitia chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba hali ya afya ya Jesus de Miguel ilizidi kuwa mbaya katika upande wa mfumo wa neva, baada ya mchezaji huyo kubaki chini ya uangalizi katika hospitali hiyo.

“Tukiwa tumevunjika moyo kwa huzuni, tukiwa na fundo kooni na tukishindwa kuamini kwamba jambo hili ni kweli, CD Tenerife inatangaza kifo cha Jesús de Miguel Alameda kilichotokea Jumanne, Novemba 3, 2026, saa 2:00 asubuhi,” ilisema taarifa ya klabu hiyo na kuongeza:

   “Hakuna maneno yanayoweza kutufariji; hakuna kabisa jambo linaloweza kupunguza maumivu haya yaliyojaa huzuni. Tunasimama pamoja na familia yake iliyokumbwa na msiba huu mkubwa, wapendwa wake na mashabiki wote wa Tenerife ambao leo wanalia.”

Kwa mujibu wa taarifa za chombo cha habari cha Marca nchini Hispania, De Miguel alidaiwa kupata mshtuko wa moyo akiwa safarini kupelekwa hospitali na ilibidi afanyiwe huduma za kumrejesha katika hali ya kawaida ndani ya gari la wagonjwa.

KIF 02

Ripoti hizo zinaeleza kuwa licha ya hali yake kutengamaa, mshambuliaji huyo bado alikuwa hajapata fahamu, ingawa alikuwa akipumua vizuri.

Tukio hilo lilitokea dakika ya saba ya nyongeza, wakati De Miguel akijaribu kuanzisha shambulizi la kushtukiza kwa upande wa Tenerife baada ya kuupokea mpira mrefu.

Hata hivyo, katika harakati za kuokoa lango lake, kipa Owono aliruka kuondoa mpira lakini goti lake lilionekana kumpiga De Miguel kifuani.

Mshambuliaji huyo alionekana kuumia na kujiviringisha chini kabla ya baadaye kutulia bila kusogea, jambo lililowalazimu madaktari kukimbilia uwanjani kutoa huduma.

Kwa zaidi ya dakika tano wahudumu wa afya walikuwa wakipambana kuokoa hali ya mchezaji huyo huku wachezaji wenzake wakionekana kushtushwa na tukio hilo. Baadhi yao walionekana wakitokwa na machozi.

Kipa Owono alionyeshwa kadi nyekundu kufuatia tukio hilo, kabla ya mwamuzi kuamua kuumaliza mchezo kutokana na uzito wa hali iliyokuwa ikiendelea.

Uwanja mzima ulitawaliwa na ukimya wakati De Miguel akipatiwa matibabu, lakini alipoondolewa kwa machela, mashabiki walimuaga kwa makofi ya heshima wakiwa wamesimama.