Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Solskjaer: Amorim? Tatizo siyo yeye

Muktasari:

  • Man United imekuwa kwenye kiwango duni tangu ilipokuwa chini ya Mreno huyo aliyekuja kuchukua mikoba ya Erik ten Hag huko Old Trafford. Amorim ameshinda mechi tano tu kati ya 16 alizoiongoza timu hiyo kwenye Ligi Kuu England, huku kikosi hicho kikishika nafasi ya 14 kwenye msimamo.

MANCHESTER, ENGLAND: OLE Gunnar Solskjaer amefichua na kusema anajua ni wapi penye shinda kwenye kikosi cha Manchester United kinachofanya hovyo chini ya Ruben Amorim na kudai sio kosa la kocha.

Man United imekuwa kwenye kiwango duni tangu ilipokuwa chini ya Mreno huyo aliyekuja kuchukua mikoba ya Erik ten Hag huko Old Trafford. Amorim ameshinda mechi tano tu kati ya 16 alizoiongoza timu hiyo kwenye Ligi Kuu England, huku kikosi hicho kikishika nafasi ya 14 kwenye msimamo.

Wachezaji kibao wa Man United wanapambana na hali kufiti kwenye mtindo wa kiuchezaji wa kocha Amorim wa 3-4-2-1. Na Solskjaer, ambaye alikuwa straika wa Man United kabla ya kuwa kocha wa miamba hiyo ya Old Trafford anachoamini ni kwamba tatizo linaanzia kwa wachezaji sio kwa Amorim ni makocha waliomtangulia.

Alipoulizwa kwa nini kuna kufukuzana sana Man United au huo ndio utamaduni wao, Solskjaer alijibu: “Hiyo ni kwa mabosi wa juu wa Man United, lakini ishu pale ni kocha kutumia wachezaji waliosajiliwa na makocha wengine.

“Nakumbuka nyakati nzuri nilipokuwa Man United nje ya zile wiki sita za mwisho. Watu wao ni safi na utamaduni ni watu. Kurudi Man United ni kama kurudi kwa familia tangu.. kama vile nilikuwepo tu muda wote.

“Lakini hapa Besiktas najiona kama familia pia, watu wanaheshimiana sana. Kuna watu hapa wamekuwa na timu hiyo kwa miaka 10, 20 hadi 30.”

Solskjaer, 52, aliinoa Man United karibu miaka mitatu, hakubeba taji hadi hapo alifunguliwa mlango wa kutokea Novemba 2021 kufuatia kichapo cha kushtua kutoka kwa Watford. Na wakati mambo yakienda kombo kwa Solskjaer alipokuwa Man United, mwenyewe anajivunia kwa kile alichokifanya kwenye timu hiyo licha ya changamoto zote.

“Zile wiki sita za mwisho zilikuwa ngumu sana, siwezi kukataa, lakini tulikuwa vinara kwenye kundi letu la Ligi ya Mabingwa Ulaya,” alisema Solskjaer.

“Ni zile mechi mbili dhidi ya Man City na Watford ndizo zilizotibua, lakini nilipambana timu ilimaliza nafasi ya pili na tatu katika misimu yangu miwili mizima niliyokuwa kwenye timu na Man United haikuwa mbaya sana kwenye Ligi Kuu England.

“Tulifika fainali ya Europa, lakini niliona pia Jose (Mourinho) aliposema mafanikio yake makubwa aliyopata Man United ni kuifanya timu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi.”

Ukirudi kwenye kikosi hicho kwa sasa, kocha Amorim anakabiliwa na mtihani mzito, kwanza wa kuikabili Fulham kwenye Kombe la FA, Jumapili kabla ya kukipiga na Real Sociedad kwenye mtoano wa Europa League, Alhamisi na baadaye kukabiliana na Arsenal kwenye Ligi Kuu England Jumapili ijayo.