Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot apiga mkwara, Liverpool ikiongoza msimamo EPL

Muktasari:

  • Maisha ya Slot yameanza vizuri sana kwenye kikosi hicho cha Merseyside. Kiwango bora cha timu yake hakimfanyi kocha huyo kubweteka. Hata wachezaji nao hawaruhusiwi kuona kama wamemaliza hivi kutokana na mafanikio yao ya uwanja kwa sasa.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL ipo kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Inaongoza pia msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini, kocha wao Arne Slot anapiga mikwara kwa kusema hapo bado hawajajipata, hawajafika kwenye ubora unaoutaka.

Maisha ya Slot yameanza vizuri sana kwenye kikosi hicho cha Merseyside. Kiwango bora cha timu yake hakimfanyi kocha huyo kubweteka. Hata wachezaji nao hawaruhusiwi kuona kama wamemaliza hivi kutokana na mafanikio yao ya uwanja kwa sasa.

Kabla ya mechi yao ya jana Jumamosi dhidi ya Fulham uwanjani Anfield, Liverpool ilikuwa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi nne, huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi na imejiweka pazuri kwenye kufuzu hatua ya mtoano ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Imetinga robo fainali ya Kombe la Ligi na itakipiga dhidi ya Southampton mwezi ujao. Mo Salah amekuwa kwenye kiwango bora sana msimu huu. Amefunga mabao 16, huku 13 yakiwa kwenye Ligi Kuu England kabla ya mechi ya jana na ameasisti mara 12 pia.

Beki Virgil van Dijk naye amekuwa kwenye kiwango bora sana katika safu ya ulinzi, Ryan Gravenberch anafanya mapinduzi makubwa kwenye safu ya kiungo, akicheza Namba 6 huku wakali kama Alexis Mac Allister na Curtis Jones nao wakiwa kwenye viwango vitamu kabisa.

Lakini, kuna mambo matamu zaidi yanakuja kutoka kwa Dominik Szoboszlai, wakati Harvey Elliott akiwa fiti kabisa na kurejea kwenye kikosi hicho, sambamba na mkali Diogo Jota huku mchezaji Federico Chiesa naye akisubiriwa kwa hamu kuonyesha ubora wake.

“Hatupo vizuri sana ila tunafanya vizuri,”  alisema Slot akizungumza kiwango bora cha timu yake na mwanzo mzuri wa timu yake.

“Nadhani kuna mambo matamu zaidi yanakuja kutoka kwa wachezaji kutoka kwenye hiki wanachokionyesha kwa sasa. Nadhani ni kitu cha kawaida kwa kila kocha. Kwa kadri unavyokaa muda mrefu timu yako inakuwa bora na inakuwa vizuri zaidi kwa wachezaji kucheza pamoja muda mrefu. Kama timu kuna mambo mazuri zaidi yanakuja. Kingine ni umri wa wachezaji ni kitu bora nilichokiri kwenye hiki kikosi, wengi wao bado vijana, hivyo ni kawaida yapo mengi mazuri yanakuja mbele.”

Kutokana na wachezaji wengine waliokuwa majeruhi wamekuwa fiti na kurejea kwenye kikosi, jambo hilo linamfanya kocha Slot kuwa kwenye presha kubwa juu ya namna atakavyopanga kikosi chako, ikianzia kwenye mchezo wa jana dhidi ya Fulham.

“Kwenye msimu huu majeruhi walikuwa Harvey, Alisson, Jota na sasa wapo fiti. Tunahitaji kikosi ambacho kipo fiti na ndio maana tunahitaji wachezaji kama Harvey na Wataru (Endo) wawe fiti. Wachezaji hawa tunawahitaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mzunguko wa pili wa ligi, ni wakati mwafaka, tunawahitaji sana,” alisema Slot.