Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Roma, Man United hakijaeleweka kwa Joshua Zirkzee

Muktasari:

  • Inaelezwa Man United inataka dau linalokadiriwa kufikia Pauni 35 milioni na hawataki kumwachia kwa mkopo kama ambavyo Roma inahitaji.

MANCHESTER United na AS Roma ziko mbali sana kufikia makubaliano ya dili la mshambuliaji raia wa Uholanzi, Joshua Zirkzee, mwenye umri wa miaka 24.

Inaelezwa Man United inataka dau linalokadiriwa kufikia Pauni 35 milioni na hawataki kumwachia kwa mkopo kama ambavyo Roma inahitaji.

Roma imekuwa ikimtaka Zirkzee ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji, lakini gharama kubwa pamoja na msimamo mkali wa United vinaifanya dili hilo kuwa na hati hati ya kufanikiwa.

Zirkzee amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika viunga vya Old Trafford, hali inayozidi kuchochea tetesi za kuondoka kwake.

Mkataba wa sasa wa Zirkzee unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 11 za michuano yote na kufunga bao moja.

Hata hivyo, mechi nyingi alizocheza aliingizwa akitokea benchi jambo ambalo halimpendezi akiamini anatakiwa kuanza ili kuongeza asilimia za kuwa mmoja wa mastaa wa Uholanzi watakaoitwa kucheza Kombe la Dunia mwakani.


Pau Torres

BARCELONA wanaangalia uwezekano wa kusajili beki wa kati katika dirish lijalo la majira ya kiangazi ili kuimarisha safu yao ya ulinzi. Pau Torres mwenye umri wa miaka 28 anayeichezea Aston Villa na timu ya taifa ya Hispania, pamoja na Nico Schlotterbeck, 26, wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Ujerumani wanatajwa kuwa mabeki waliopo katika rada zao. Barcelona imevutiwa sana na mabeki hawa kwa sababu wana uwezo mkubwa wa kujenga mashambulizi kuanzia nyuma.


Kobbie Mainoo

CHELSEA imeweka kipaumbele cha kuimarisha safu yao ya kiungo wa kati dirisha la usajili wa majira ya kiangazi na tayari ina majina mawili ya mastaa ambao imepanga kuwasajili. Mastaa hao ni pamoja na Kobbie Mainoo, 20, wa Manchester United na Adam Wharton, 21, wa Crystal Palace. Chelsea inaamini kusajili viungo wenye umri mdogo  itasaidia kuleta ushindani wa namba na timu kufanya vizuri.


Daniel Munoz

CRYSTAL Palace inaangalia uwezekano wa kusajili beki wa kulia katika dirisha la usajili la Januari, baada ya beki wao Daniel Munoz kupata majeraha yanayoweza kumuweka nje kwa muda mrefu. Munoz, 29 na raia wa Colombia, anatarajiwa kukosa michezo mingi hali iliyolazimisha Palace kuanza kutafuta mbadala wake mapema. Awali staa huyu tegemeo alikuwa akihusishwa kutaka kusajiliwa na baadhi ya vigogo wa England lakini majeraha hayo yameripotiwa kusitisha kika kitu.


Marc Guehi

KOCHA wa Crystal Palace, Oliver Glasner anaamini beki wao wa kimataifa wa England, Marc Guehi, 25,  atabaki katika kikosi hadi mwisho wa msimu huu na mkataba wake unatarajiwa kumalizika. Licha ya tetesi za kuhusishwa na klabu kubwa, Glasner anaamini Guehi ataendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi hadi msimu utakapomalizika na baada ya hapo anaweza kuondoka. Kocha huyu ndiye aliyeingilia kati dili la Guehi la kwenda Liverpool dirisha lililopita la majira ya kiangazi na ilionekana kuwa na asilimia zaidi ya 70 za kukamilika.


Niclas Fullkrug

AC MILAN wako katika mazungumzo na West Ham United ili kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Ujerumani Niclas Fullkrug, mwenye umri wa miaka 32. Inadaiwa Milan wamependekeza dili la mkopo wenye kipengele cha kumnunua mazima mwisho wa msimu ikiwa itaridhishwa na kiwango chake. Milan inaamini Fullkrug ambaye sio tegemeo kwa sasa katika kikosi cha West Ham anaweza kuongeza nguvu na uzoefu katika safu yao ya ushambuliaji.


Santiago Gimenez

LEEDS United hawana mpango wa kutumia kiasi cha zaidi Pauni 25 milioni kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na timu ya taifa ya Mexico, Santiago Gimenez, mwenye umri wa miaka 24, kwani inaona kiasi hicho cha pesa ni kikubwa kwao. Hata hivyo, Leeds inataka kujaribu kuomba kumsajili kwa mkopo wa muda mfupi dirisha la usajili la Januari lakini kuwepo kwa kipengele cha kumnunua mazima mwisho wa msimu. Santiago ameomba kuondoka mwenyewe ili kujaribu changamoto mpya mahali kwingine kwani hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza.


Kevin Filling

MANCHESTER United ipo katika vita kali dhidi ya Borussia Dortmund na timu nyingine Ulaya katika harakati za kutaka kumsajili mshambuluaji kinda kutoka Sweden, Kevin Filling mwenye miaka 19 anayeichezea AIK Fotboll. Filling amekuwa akitazamwa na maskauti wa timu nyingi barani Ulaya ambao wote wameonyesha kuvutiwa na kiwango chake. Kinda huyu amekuwa aiifananishws sana na Alexander Isak wa Liverpool kutokana na aina ya uchezaji wake pamoja na umbo alilonalo.