Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shuti la Lionel Messi laharibu kamera ya mpigapicha!

MESSI Pict

Muktasari:

  • Matukio ya aina hiyo si ya kawaida, hata kwa mchezaji kama Messi. Kuwa karibu naye mara nyingi humaanisha kushuhudia ubora wa hali ya juu wa soka lake, lakini safari hii kumbukumbu iliyobaki ilikuwa ya kipekee ikiwa ni simulizi nyingine ya kuvutia ndani ya dunia ya Inter Miami.

MIAMI, MAREKANI: UNAPOMUONA Lionel Messi akijiandaa kupiga shuti na wewe uko nyuma ya goli ukiwa na kamera mkononi elewa kwamba unajiandalia balaa kwani unaweza kunasa picha ya kipekee au ukajikuta unaharibu kifaa chakocha kuchukulia picha.

Mpigapicha mmoja wakati wa mazoezi ya Inter Miami kilichotokea ni tukio la pili na ndicho kilicholeta mjadala.

Inter Miami tayari ilikuwa ikifuatiliwa na vyombo vya habari kuelekea mchezo dhidi ya New York Red Bulls, lakini tukio  la mazoezini lilimweka Messi tena katikati ya mjadala, kwani shuti kali kutoka kwa nyota huyo wa Argentina lilizua tukio lisilotarajiwa ambalo lilianza kusambaa haraka mitandaoni.

Shuti hilo halikwenda moja kwa moja golini kama ilivyotarajiwa na badala yake mpira ulibadili mwelekeo baada ya kugonga kitu na kuishia kuigonga kamera ya mpigapicha iliyokuwa umbali wa mita chache kutoka tukio hilo.

Kinachodaiwa ni nguvu ya shuti hilo ilikuwa kubwa kiasi cha kuharibu lenzi ya kamera, jambo lililomshangaza mpigapicha huyo.

Mwandishi mmoja aliyekuwa karibu alifanikiwa kunasa tukio hilo na katika picha hizo inaonekana wakati mpira unapogonga kifaa hicho pamoja na mshangao wa mpigapicha alipogundua kuwa kamera yake ikiharibika hata kabla ya mechi kuanza.

Matukio ya aina hiyo si ya kawaida, hata kwa mchezaji kama Messi. Kuwa karibu naye mara nyingi humaanisha kushuhudia ubora wa hali ya juu wa soka lake, lakini safari hii kumbukumbu iliyobaki ilikuwa ya kipekee ikiwa ni simulizi nyingine ya kuvutia ndani ya dunia ya Inter Miami.