Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi alivyofunika rekodi ya Pele mipira ya free-kick

MESSI Pict

Muktasari:

  • Rekodi za nje ya uwanja ni zile zinazohusiana na maisha binafsi ikiwamo utajiri, huduma za jamii anazotoa na misaada anayotoa na kadhalika.

WASHINGTON, MAREKANI: NAHODHA wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi anaendelea kuvunja rekodi mbalimbali na tangu alipoanza soka la ushindani zaidi ya miaka 20 iliyopita tayari keshazivunja zaidi ya 30 za nje na ndani ya uwanja.

Rekodi za nje ya uwanja ni zile zinazohusiana na maisha binafsi ikiwamo utajiri, huduma za jamii anazotoa na misaada anayotoa na kadhalika.

MESS 01

NDANI YA UWANJA KUNA MENGI.

Kwa ufupi ni kwamba Messi ndiye mwanasoka pekee aliyebeba tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon D’or) mara nane akifuatiwa na mpinzani wake wa siku nyingi, Cristiano Ronaldo aliyebeba mara tano.

Si hivyo tu, lakini kwa sasa amefikisha mabao 900 ya kufunga akizitumikia timu mbalimbali alizocheza pamoja na ile ya taifa, huku kukiwa na mabao kibao ambayo hayapo katika mfumo wa rasmi kwa kuwa aliyafunga utotoni wakati huo akicheza mitaani.

Lakini, wakati unatafakari juu ya mchezaji huyo taarifa za karibuni zinaonyesha kwamba yupo karibu zaidi kuliko wakati wowote ule kutawazwa  kuwa mfalme wa mipira ya adhabu (free-kick) katika soka.

Messi aliingia kwenye orodha ya wafungaji kwa klabu yake ya Inter Miami waliporudi kutoka nyuma na kuifunga New York City mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu Marekani (MLS), wiki tatu zilizopita.

Na ni katika mchezo huo alipofanya jambo la ajabu kwani mshindi huyo wa Kombe la Dunia alifunga dakika ya 61, ikiwa ni bao lake la nne katika idadi sawa ya mechi za ligi msimu huu.

Hata hivyo, halikuwa bao la kawaida tu. Messi alifunga kwa mkwaju wa faulo kutoka umbali wa mita 30 uliomgonga beki wa New York na kumbabatiza kipa Matt Freese aliyekuwa hana la kufanya. Hilo lilikuwa bao la 901 katika maisha yake yenye mafanikio makubwa, na la kuvutia zaidi ikiwa ni free-kick yake ya 71 aliyofunga.

MESS 02

ZAIDI YA PELE

Idadi ya free-kick za Messi sasa imemzidi Pele, ambaye alifunga 70 katika maisha yake.

Licha ya ubora wake katika mipira ya adhabu, bado Messi anahitaji mabao machache ili kuchukua rekodi hiyo kabisa.

Rekodi hiyo bado inashikiliwa na gwiji wa Brazil, Juninho Pernambucano, ambaye alifunga free-kick 77 katika maisha yake ya soka. Hii ina maana Messi anahitaji kufunga free-kick sita ili kufikia rekodi hiyo na saba ili kuivunja.

Fursa iliyofuata kwa Messi kuongeza idadi yake ya free-kick ilikuwa Machi 27, ambapo Argentina ilicheza dhidi ya Mauritania katika mechi ya kirafiki, lakini hakufunga kwani walikuwa ni Enzo Fernandez and Nico Paz waliotupia kwa nchi yake. Lakini, Argentina, mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia watahitimisha mechi za kimataifa za kalenda ya Fifa, leo dhidi ya Zambia.

Katika timu ya taifa, Messi amevunja rekodi kibao kwa Argentina ikiwamo ufungaji mabao ambapo alimvuka Gabriel Batistuta aliyeondoka na mabao 54 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Argentina akifikisha 115 katika mechi 197.

Vilevile ana rekodi yake Amerika Kusini ambako sasa amemvuka Pele aliyekuwa kinara wa bara na mabao 77 na kuwa mfungaji bora zaidi kwa timu za taifa Amerika Kusini, ilhali upande wa Kombe la Dunia 2022 alifunga mabao saba na kutoa asisti saba akiiongoza Argentina kushika nafasi ya tatu.

MESS 03

INTER MIAMI vs MESSI

Kocha wa Inter Miami, Javier Mascherano ambaye gwiji wa Argentina pia amekuwa akimhitaji Messi kutokana na uwezo wake wa kuamua mechi kubwa kwa njia mbalimbali ikiwamo free-kick na anaamini bila uwapo wake uwanjani mambo huwa magumu kwao.

Mascherano anasema kikosi hicho kinapokuwa na Messi katika ubora wake kila wanachopanga hufanikiwa, kwani ni aina ya wachezaji mafundi wanaoweza kuamua mchezo kwa ushindi dhidi ya wapinzani wao.

Anasema wanaamini kwamba “haiwezekani” kwa timu hiyo kufikia malengo bila yeye, na hilo limekuwapo kwa muda mrefu sasa.

“Tunajaribu kumtunza Leo kadri iwezekanavyo. Anajisikia vizuri kucheza. Sasa yupo kwenye timu ya taifa, na atakaporejea tutaona hali itakuwaje. Ni mchezaji muhimu kufikia malengo yetu. Bila yeye, haiwezekani,” anasema kocha huyo.

Ushindi wa Inter Miami kabla ya kwenda kwenye mapumziko ya kalenda ya Fifa umeiweka katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ukanda wa Mashariki wa MLS ikiwa na pointi 10 zikiwa ni tatu nyuma ya vinara Nashville. Timu hiyo itarejea kwenye mechi za ligi Aprili 5 itakapoikaribisha Austin.