Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shujaa wa Chelsea ashangazwa na Trump

TRUMP Pict

Muktasari:

  • Trump (79), akiwa ameambatana na mkewe Melania na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, alikuwa miongoni mwa wageni wa heshima walioketi eneo la watu maarufu (VIP) kushuhudia mchezo huo.

SHUJAA wa Chelsea, Cole Palmer, amefunguka kuhusu kitendo kilichowashangaza wengi kutokana na uwepo wa Rais wa Marekani, Donald Trump, wakati wakisherehekea kutwaa Kombe la Dunia la Klabu, jana Jumapili.

Trump (79), akiwa ameambatana na mkewe Melania na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, alikuwa miongoni mwa wageni wa heshima walioketi eneo la watu maarufu (VIP) kushuhudia mchezo huo.

Hata hivyo, tofauti na matarajio, baada ya kumkabidhi kombe nahodha wa Chelsea, Reece James, Trump hakurudi nyuma kama ilivyo desturi. 

Badala yake, aligoma kushuka jukwaani na kuendelea kusimama mbele ya kamera huku akipiga picha na wachezaji, kitendo kilichowaacha mastaa wa Chelsea katika hali ya mshangao.

Palmer, ambaye alifunga mabao mawili katika mchezo huo na kutoa asisti bao la tatu, alinaswa na kamera akionekana kutofurahishwa na tukio hilo huku akisikika akisema: “Anafanya nini huyu?"

Akizungumza baadaye na BBC Sport kupitia mwandishi Nizaar Kinsella, Palmer alisema: "Nilijua kwamba atakuwepo uwanjani lakini sikujua kama atapanda jukwaani wakati tunapokea kombe. Kwa hiyo nilishangaa sana."

TRU 01

Hali hiyo ilijirudia pia wakati Trump alipomkabidhi Palmer tuzo ya mpira wa dhahabu (Golden Ball), ambapo kiungo huyo mwenye miaka 23 alionekana bado kuwa na mshangao usoni.

Baada ya kukabidhi medali kwa timu zote mbili Chelsea na PSG,  Trump alisalia jukwaani katikati kabisa huku wachezaji wa Chelsea wakinyanyua kombe, licha ya kuombwa na Infantino kushuka.

Tukio hilo limeibua gumzo kubwa mitandaoni na katika vyombo vya habari, wengi wakisema Rais huyo wa Marekani "aliiba shoo" isivyotarajiwa, huku wengine wakiona ni ukiukaji wa taratibu za soka na heshima ya tukio hilo la kihistoria.