Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serena, Venus walivyorudi na kijiji Cicinnati Open

WILLIAMS Pict

Muktasari:

  • Kina Williams wamecheza mchezo wa kwanza wawili wawili tangu 2022 walipoamua kujiweka kando na tenisi na kujikita katika mambo mengine nje ya uwanja ikiwamo malezi ya familia. Katika mchezo huo, washindi waliondoka na seti 6-2, 1-6, 10-8.

CICINNATI, MAREKANI: NDUGU wawili waliotawala michuano ya kiamtaifa ya tenisi duniani, Serena na Venus Williams wamerudi kucheza mechi za wawili wawili katika mashindano ya Cicinnati Open kwenye mchezo wa kwanza wa 'doubles' na kukubali kichapo kutoka kwa Marta Kostyuk aliyeshirikiana na Peyton Stearns.

Kina Williams wamecheza mchezo wa kwanza wawili wawili tangu 2022 walipoamua kujiweka kando na tenisi na kujikita katika mambo mengine nje ya uwanja ikiwamo malezi ya familia. Katika mchezo huo, washindi waliondoka na seti 6-2, 1-6, 10-8.

Hata hivyo, kwa kina Serena na Venus ilikuwa ni “burudani” ya kurejea pamoja uwanjani licha ya kichapo, kwani muungano huo wa kifamilia ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tenisi.

Baada ya kuanza kwa mchezo Venus aliruka kwenye mstari wa nyuma wa uwanja akifuatilia kwa umakini mpira wa pili dhaifu wa wapinzani wao na kuibua shangwe la mashabiki ambao waliikosa mikimbio yake katika mashindano makubwa.

WILL 01

Kwa muda mfupi, Uwanja wa Grandstand katika mashindano ya Cincinnati Open ulionekana kama umerudi miaka 15 nyuma ambapo walitawala tenisi kiasi cha kupishana mara kwa mara katika nafasi mbili za juu za ubora duniani.

Baada ya hapo Venus alipiga kwa nguvu mpira kwa pigo la 'forehand' moja kwa moja kuelekea kwenye nyonga ya kulia ya mpinzani wake, Marta, na kuongeza mayowe kwa mashabiki.

Enzi zile ambapo kinadada hao walitumia muda wao wa mapumziko kukusanya mataji ya Grand Slam kana kwamba ni jambo la kawaida, hivi ndivyo walivyowashughulikia wapinzani wao wengi.

Hata hivyo, mwisho wa mchezo, pambano la kwanza la doubles kwa Venus na Serena katika kipindi cha miaka minne na la pili pekee katika muongo mmoja uliopita kwao liliishia kwa kushindwa kwa seti 6-2, 1-6, 10-8 dhidi ya Kostyuk na Peyton, ambao pia walipata nafasi ya kushiriki mashindano hayo kwa wildcard (upendeleo maalumu) na ni wachezaji wawili wenye uwezo mkubwa katika mchezo wa mtu mmoja mmoja.

WILL 02

Lakini, matokeo hayakuonekana kuwa na umuhimu mkubwa kwa wachezaji wote wanne kwani ilikuwa kama kukumbushia enzi zao, kwani hata baada ya mchezo mazungumzo yalilenga zaidi katika kufurahia dakika walizokuwa pamoja kuwaburudisha mashabiki wao.

“Ni wazi kwamba kushinda ni jambo zuri,” amesema Serena na kuongeza:

“Lakini nadhani katika nafasi hii, tunajaribu tu kufurahia. Sikuja hapa kwa lengo la kushinda mashindano haya. Bila shaka nilitaka kufanya vizuri kadiri nilivyoweza, lakini nadhani muhimu ni kufurahia na pia kuona hali zetu zipoje, jinsi tunavyojisikia tukiwa uwanjani. Kuwa uwanjani pamoja na mashabiki pia ni jambo zuri sana, kwa sababu tunawapa tena nafasi ya kutuona tukicheza, jambo ambalo ni la kipekee.”

Hata kabla Serena hajafanya safari yake ya kawaida kwenda Mason, Ohio, uwepo wake ulikuwa tayari umeonekana katika viwanja vya mashindano hayo mwaka huu. Kwa siku mbili wakati wa raundi ya kwanza, ndege ilizunguka juu ya viwanja vya mashindano ikiwa imebeba bango la matangazo ya Serena akiitangaza Ro, kampuni ya huduma za afya kwa njia ya mtandao inayowawezesha wagonjwa kupata dawa za kupunguza uzito aina ya GLP-1.

WILL 03

Mchezo huo pia ulionyesha kwa namna ya kipekee jinsi ambavyo tenisi ya kulipwa bado inaweza kuwa na changamoto. Licha ya hamasa kubwa iliyozunguka kurejea kwa kinadada hao ambao kwa karibu kabisa huenda hii ikawa mara ya mwisho kwa mashabiki kuwaona wakicheza pamoja, masharti magumu ya mikataba ya televisheni yalisababisha mchezo huo kupelekwa kwenye Uwanja wa Grandstand, ukiwa ni wa pili wa mashindano hayo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 5,000.

Kila kiti kilikuwa na mtu, huku mashabiki wakiingia na kujazana kwenye ngazi ili kupata nafasi ya kuwaona nyota hao wawili wakubwa wa Marekani. Licha ya furaha, msisimko na hamu ya kuwaona tena wakiwa pamoja, mwanzo wa mchezo wenyewe haukuwa mzuri sana.

Kutokuwa na mechi za kutosha kwa Serena kulionekana kuwa tatizo kubwa zaidi, huku mdogo wake akishindwa kupata muda sahihi wa kupiga mipira yake ya kawaida kutoka nyuma ya uwanja na pia kukosa ubora wa kuokoa jambo ambalo kawaida huwa bora kwa mastaa wa kiwango chake.

Kadiri Serena alivyoanza kuondokana na udhaifu mchezoni, Venus naye aliendelea kucheza kwa utulivu, akichanganya upigaji mzuri wa mipira. Kufikia mwanzo wa seti ya pili, kila kitu kilianza kwenda sawa. Kinadada hao walitawala seti ya pili na kulazimisha mchezo kuingia kwenye 'match tie-break'.

Wakiwa nyuma kwa 2-8 katika tie-break hiyo, Serena na Venus walikaribia kufanya mageuzi makubwa ya matokeo baada ya kuanza kurejea kwa kasi. Hata hivyo, 'double fault' ya Venus wakati walipokuwa nyuma kwa 8-9 ilimaliza matumaini yao ya kuibuka na ushindi.