Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namungo yaota pointi sita nyumbani

NAMUNGO Pict
NAMUNGO Pict

Muktasari:

  • Masoud amesema ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TRA United katika mchezo uliopita umeongeza matumaini ya kuendelea na matokeo mazuri, huku akisisitiza umuhimu wa kutumia vizuri mechi za nyumbani baada ya kupoteza  nne mfululizo ugenini.

BEKI wa Namungo, Hance Masoud anaamini timu hiyo itavuna pointi sita katika michezo miwili ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania nyumbani.

Masoud amesema ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TRA United katika mchezo uliopita umeongeza matumaini ya kuendelea na matokeo mazuri, huku akisisitiza umuhimu wa kutumia vizuri mechi za nyumbani baada ya kupoteza  nne mfululizo ugenini.

“Tulifanya vibaya na haikuwa lengo letu, hivyo tunataka kutumia vizuri mechi zetu za nyumbani. Moja tumeshinda, bado mbili ili kuweka vizuri hesabu zetu katika michezo hii ya mwanzoni mwa msimu,”  amesema Masoud.

Beki huyo anafahamu kuwa michezo hiyo haitakuwa rahisi, lakini anaamini maandalizi mazuri na kutumia vyema faida ya kucheza nyumbani kutakuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha lengo lao la kupata pointi zote sita.

“Ligi ni ngumu, hivyo ni muhimu kutumia faida ya kucheza nyumbani. Najua mechi hizo hazitakuwa nyepesi, ila naamini tutafanya vizuri,”  amesema.

Ushindi dhidi ya TRA United umeifanya Namungo kufikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi nane, ikiwa imeshinda mara tatu na kukaa katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara. Kwa timu hiyo ya Ruangwa, mechi dhidi ya Coastal Union Oktoba 24 na Polisi Tanzania Oktoba 29, 2026 ni fursa ya kuongeza pointi.