Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twiga Stars yang’ara FIFA

TWIGA Pict

Muktasari:

  • Twiga Stars imepanda kutoka nafasi ya 122 iliyokuwepo awali hadi katika nafasi ya 111.

TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imepanda kwa nafasi 11 katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwezi Oktoba.

Twiga Stars imepanda kutoka nafasi ya 122 iliyokuwepo awali hadi katika nafasi ya 111.

Ushiriki wa Twiga Stars katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) zilizofanyika Morocco kuanzia Julai 26 hadi Agosti 16 mwaka huu, umeonekana kuibeba Twiga Stars na kuiwezesha kupanda katika viwango hivyo vya ubora.

Katika mashindano hayo, Twiga Stars iliambulia pointi moja katika mechi tatu, lakini sare yenyewe ilikuwa dhidi ya Afrika Kusini ‘Banyana Banyana’ ambayo kidunia iko katika nafasi ya 59.

Twiga Stars kwa mwezi Oktoba, imekusanya pointi 1164.03 ambazo zimeipaisha kwa nafasi hizo 11.

Malawi ndio timu iliyopanda kwa nafasi nyingi zaidi kwenye viwango hivyo vya ubora wa soka la wanawake ambapo imepanda kwa nafasi 49.

Awali, Malawi ilikuwa katika nafasi ya 153 hadi katika nafasi ya 104.

Kufanya vizuri kwa Malawi katika fainali za WAFCON ambapo ilifika hatua ya fainali, kumechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya Malawi itambe katika viwango vya ubora kwa mwezi Oktoba.

Hispania imeendelea kuongoza duniani ikifuatiwa na Marekani, huku Ujerumani ikishika nafasi ya tano.

England inayoshika nafasi ya nne na Japan ambayo ipo katika nafasi ya tano zinakamilisha orodha ya timu tano vinara kwenye chati hiyo.