Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya Liverpool, Salah aanza safari mpya Trabzonspor

Muktasari:

  • Tayari Salah amewasili Uturuki kwa ajili ya kukamilisha hatua za mwisho ikiwemo utambulisho kufuatia vipimo vya afya kufanyika.

TRABZON, UTURUKI: BAADA ya miezi kadhaa ya sintofahamu kuhusu hatima yake tangu aondoke Liverpool, mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, amejiunga na Trabzonspor ya Uturuki.

Tayari Salah amewasili Uturuki kwa ajili ya kukamilisha hatua za mwisho ikiwemo utambulisho kufuatia vipimo vya afya kufanyika.

Klabu hiyo imeeleza kuwa, baada ya kuwasili, Salah ataelekea mji wa Trabzon ambako atakutana na viongozi wa klabu na kukamilisha mchakato wa kutambulishwa rasmi mbele ya mashabiki.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka nchini Uturuki, Trabzonspor imempa nyota huyo mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya takribani euro milioni 17 (zaidi ya Sh50 bilioni za Kitanzania).

Kabla ya Trabzonspor kuingia kwenye mbio hizo, Salah alikuwa akihusishwa kwa nguvu na Beşiktaş.

Hata hivyo, mazungumzo kati ya pande hizo yalivunjika baada ya kushindwa kufikia mwafaka kuhusu masuala ya kifedha.

Mkurugenzi wa Beşiktaş, Önder Özen, alikiri kuwa walifanya mazungumzo kadhaa na Salah pamoja na wawakilishi wake, lakini mazungumzo yalikwama baada ya upande wa fedha kuwa kikwazo kikubwa.

Aidha, alisema wakati huo mchezaji huyo alikuwa pia akitafutwa na klabu kutoka Saudi Arabia pamoja na Ligi Kuu ya Marekani (MLS).

Salah, mwenye umri wa miaka 34, ameondoka Liverpool baada ya kuitumikia kwa misimu tisa tangu alipojiunga akitokea Roma mwaka 2017.

Katika kipindi hicho aliweka historia kubwa kwa kufunga mabao 257 katika mechi 442 na kuwa mfungaji wa tatu bora wa muda wote wa klabu hiyo.

Pia alisaidia Liverpool kutwaa mataji makubwa ikiwemo Ligi Kuu England mara mbili, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia la Klabu na mataji mengine ya ndani.

Kwa mafanikio binafsi, Salah alitwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu England mara nne na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England (PFA) mara tatu.