Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo ana magari ya Sh80 bilioni

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno na mshambuliaji wa Al-Nassr alichapisha picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa amesimama ndani ya gereji yake, huku nyuma yake kukiwa na baadhi ya magari yake ya kifahari yakiwemo Ferrari mbili nyekundu na Bugatti. Picha hizo aliambatanisha na ujumbe mfupi uliosomeka, "My toys".

LONDON, ENGLAND: CRISTIANO Ronaldo ameendelea kuthibitisha kuwa yeye si mfalme wa mabao pekee, bali pia ni miongoni mwa wanamichezo wenye maisha ya kifahari zaidi duniani baada ya kuwaonyesha mashabiki wake mkusanyiko wa magari yake yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Pauni22 milioni(takribani Sh80.5 bilioni).

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno na mshambuliaji wa Al-Nassr alichapisha picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa amesimama ndani ya gereji yake, huku nyuma yake kukiwa na baadhi ya magari yake ya kifahari yakiwemo Ferrari mbili nyekundu na Bugatti. Picha hizo aliambatanisha na ujumbe mfupi uliosomeka, "My toys".

Ronaldo, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 41, amekuwa akikusanya magari ya kifahari kwa miaka mingi kiasi kwamba hata yeye mwenyewe anakiri ameshindwa kujua idadi halisi anayomiliki.

RONA 01

Akizungumza mwaka jana amesema amepoteza hesabu, lakini anaamini anamiliki magari kati ya 40 na 41, huku akisisitiza kuwa Bugatti ndiyo aina anayozipenda zaidi kwa sababu ni magari ya kipekee.

Miongoni mwa magari ya thamani kubwa zaidi katika gereji yake ni Bugatti Tourbillon lenye thamani ya Pauni milioni 3.2, ambalo ni moja ya magari mapya zaidi aliyoongeza kwenye mkusanyiko wake.

Pia anamiliki Bugatti Chiron yenye thamani ya Pauni milioni 2, Bugatti Veyron ya Pauni milioni 1.5 na Bugatti Centodieci inayokadiriwa kugharimu Pauni milioni 7.

Mbali na Bugatti, Ronaldo pia ana mkusanyiko mkubwa wa Ferrari unaojumuisha Ferrari Monza yenye thamani ya Pauni milioni 1.4, Ferrari Daytona SP3 ya Pauni milioni 2 pamoja na Ferrari Purosangue. Gereji yake pia imepambwa na magari mengine ya kifahari kama McLaren Senna ya Pauni 750,000, Lamborghini Aventador ya Pauni 270,000, Bentley Flying Spur ya Pauni 250,000, Mercedes G-Wagon Brabus ya Pauni 600,000, sambamba na magari matatu ya Rolls-Royce.

RONA 02

Aidha, wakati alipohamia Al-Nassr, Ronaldo na wachezaji wenzake walizawadiwa magari aina ya BMW na klabu hiyo, jambo lililozidi kuongeza thamani ya mkusanyiko wake wa magari.

Picha hizo zimeibua gumzo kubwa mitandaoni, huku mashabiki wengi wakivutiwa na maisha ya kifahari ya nyota huyo. Wengine walieleza kuwa huo ni mkusanyiko unaostahili mchezaji anayechukuliwa kuwa mmoja wa bora zaidi katika historia ya soka.

Mbali na kuendelea kung'ara uwanjani, Ronaldo pia anatarajiwa kuingia katika hatua mpya ya maisha yake binafsi mwishoni mwa wiki hii, ambapo anatazamiwa kufunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Georgina Rodriguez katika kisiwa cha Madeira, Ureno.

Taarifa zinaeleza kuwa harusi hiyo itafanyika katika kanisa jijini Funchal, huku mapokezi yakifanyika katika hoteli ya kifahari ya nyota tano ya Savoy Palace, mbele ya wageni mbalimbali mashuhuri kutoka duniani.