Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rice akubali miaka mitano Arsenal

RICE Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Arsenal mwaka 2023 akitokea West Ham United kwa ada ya pauni milioni 105, na tangu wakati huo amekuwa mhimili muhimu katika eneo la kiungo.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Declan Rice, amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitano utakaomuweka ndani ya kikosi cha The Gunners hadi majira ya joto ya mwaka 2031.

Rice anatarajiwa kuweka saini kwenye mkataba huo hivi karibuni, ambao utamfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi ndani ya klabu hiyo, akilingana na staa mwenzake Bukayo Saka.

Saka kwa sasa anatajwa kulipwa zaidi ya pauni 350,000 (Sh bilioni 1.1) kwa wiki, kiwango kinachoonesha thamani ya nyota hao wawili katika kikosi cha Arsenal.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Arsenal mwaka 2023 akitokea West Ham United kwa ada ya pauni milioni 105, na tangu wakati huo amekuwa mhimili muhimu katika eneo la kiungo.

RIC 01

Uwezo wake wa kukaba, kusambaza mipira na kuongoza mchezo umemfanya kuwa mmoja wa wachezaji tegemeo katika mfumo wa kocha Mikel Arteta.

Msimu uliopita, Rice alicheza jumla ya mechi 55 katika mashindano yote, akiisaidia Arsenal kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006, ingawa walipoteza kwa Paris Saint-Germain.

Mazungumzo ya mkataba mpya yalikuwa yakiendelea tangu Machi mwaka huu na sasa pande hizo mbili zimefikia makubaliano.

Awali, mkataba wa Rice na Arsenal ulikuwa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

RIC 02

Akizungumza akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya England mwishoni mwa wiki, Rice alidokeza kuwa makubaliano ya mkataba mpya yalikuwa karibu kukamilika.

"Nimekuwa na bahati kubwa kucheza katika kiwango kizuri na kwa uthabiti katika kipindi chote cha maisha yangu ya soka. Nimekuwa na utulivu katika klabu zote nilizowahi kuchezea," amesema Rice.

Ameongeza: "Natumaini mkataba mpya utapatikana hivi karibuni. Nina bahati kubwa kuwa katika klabu kama Arsenal, ambako kocha wangu Mikel Arteta na wachezaji wenzangu wananipa nguvu na kuniamini."

Hatua hiyo ni ishara nyingine ya dhamira ya Arsenal kuendelea kujenga kikosi imara kitakachoshindania mataji makubwa kwa miaka ijayo.