Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Arsenal azua la kuzua

RICE Pict

Muktasari:

  • Rice ametoa majibu hayo baada ya Souness kumkosoa kwa kile alichokiita kucheza soka la kizamani, akidai kiungo huyo anashuka mara kwa mara kucheza eneo la ulinzi badala ya kutimiza majukumu yake ya kiungo.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Declan Rice amemjibu mchambuzi wa soka, Graeme Souness, kufuatia ukosoaji wake akidai kuwa hajafahamu namna mchezo wa soka ulivyobadilika katika miaka ya hivi karibuni.

Rice ametoa majibu hayo baada ya Souness kumkosoa kwa kile alichokiita kucheza soka la kizamani, akidai kiungo huyo anashuka mara kwa mara kucheza eneo la ulinzi badala ya kutimiza majukumu yake ya kiungo.

Souness, ambaye ni kiungo wa zamani wa Liverpool, amekuwa akiamini kuwa Rice hafanyi vya kutosha katika eneo la kiungo, huku akidai kuwa angefaa zaidi kucheza kama beki wa kati na asingepata nafasi katika timu kubwa kama Real Madrid au Barcelona.

RIC 01

Hata hivyo, Rice amesema takwimu zake tangu alipojiunga na Arsenal mwaka 2023 zinajieleza zenyewe, akiwa amefunga mabao 22 na kutoa pasi 33 za mabao.

“Takwimu zangu tangu nilipojiunga na Arsenal zinajieleza zenyewe. Kwa beki wa kati, nadhani hizo si takwimu mbaya. Nimekuwa na pasi nyingi za mabao na mabao mengi. Kama ni beki wa kati wa kiwango cha juu mwenye takwimu hizo, ninafurahi sana,” amesema Rice kwa mzaha.

Kiungo huyo ameongeza kuwa amekuwa akifahamu maoni ya Souness tangu alipokuwa akiichezea West Ham United, lakini hawezi kubadili mtazamo wake na badala yake anachoweza kufanya ni kuendelea kuonyesha uwezo wake uwanjani.

“Graeme ana maoni yake. Nadhani amekuwa na mtazamo huo tangu siku zangu za West Ham. Nimeona anachokisema, lakini siwezi kubadili maoni yake. Ninachoweza kufanya ni kuingia uwanjani, kucheza vizuri, kufanya kazi yangu na kupuuza kelele,” amesema.

RIC 02

Rice pia alieleza kuwa huenda Souness, mwenye umri wa miaka 73, hajazingatia mabadiliko makubwa yaliyotokea katika mbinu za soka la kisasa, akitolea mfano mshambuliaji Harry Kane anavyoshuka nyuma kuchukua mipira karibu na mabeki wa kati.

Amesema katika mchezo waliocheza hivi karibuni dhidi ya Kane, mshambuliaji huyo alishuka mara nyingi eneo la ulinzi ili kupokea mipira na kusaidia kujenga mashambulizi.

“Mchezo umebadilika. Siku hizi unapaswa kutoka kwenye eneo lako, kwenda sehemu tofauti za uwanja ili kutengeneza nafasi, kuwazidi wapinzani kwa idadi na kupeleka mpira mbele. Soka limebadilika sana na kila wakati unatafuta namna ya kupata faida ya kiufundi,” amesema Rice.

Ameongeza kuwa amekuwa akifanya kazi kwa karibu na kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, kupitia uchambuzi wa video na maelekezo ya moja kwa moja uwanjani ili kuboresha namna anavyocheza akiwa kiungo.

Rice amesema Arteta humwelekeza namna ya kuanzisha mashambulizi akiwa nyuma, kushuka karibu na kipa au kwenda pembeni kwa ajili ya kupokea mpira na kuusogeza mbele.

RIC 03

Pamoja na kutokubaliana na ukosoaji wa Souness, Rice amesisitiza kuwa anamheshimu kutokana na mafanikio aliyoyapata akiwa mchezaji, akimtaja kuwa mmoja wa viungo bora wa kizazi chake.

Amesema hajawahi kukutana na Souness ana kwa ana, lakini akipata nafasi hiyo atamsalimia na kuzungumza naye bila tatizo, akieleza kuwa kila mmoja ana haki ya kuwa na maoni yake kuhusu soka.