Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Declan Rice ana ujumbe wako

RICE Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 amefichua kuwa aliacha kutumia mtandao wa X miaka mitatu iliyopita kutokana na wingi wa ujumbe hasi aliokuwa akikumbana nao.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Declan Rice, amefunguka kuhusu uamuzi wake wa kupunguza matumizi ya mitandao ya kijamii, akisema wakati mwingine taarifa hasi anazokutana nazo kwenye majukwaa hayo zinaweza kumharibia siku, huku akieleza kuhusu malezi bora ya watoto.

Rice, ambaye amekuwa akikabili mashambulizi ya matusi na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa mitandao, amesema amejifunza kujitenga na mambo yanayoweza kuathiri utulivu wake wa akili.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 amefichua kuwa aliacha kutumia mtandao wa X miaka mitatu iliyopita kutokana na wingi wa ujumbe hasi aliokuwa akikumbana nao.

Akizungumza na jarida la GQ, baada ya kutajwa miongoni mwa watu mashuhuri wa mwaka, Rice amesema:

RIC 01

“Bado sijarudi tena kwenye programu hiyo. Unaweza kuamka asubuhi ukiwa na furaha, lakini ukasoma jambo moja tu na ghafla siku yako nzima ikaharibika.”

Ameongeza kuwa uwezo wake mkubwa ni kujitenga na kelele zisizo na manufaa na kutokubali mambo yasiyomjenga kumuingilia.

Mchezaji huyo pia amewahi kushuhudia mwenza wake wa muda mrefu, Lauren Fryer, akilengwa na mashambulizi ya mtandaoni kuhusu muonekano wake, hali iliyomfanya kufuta machapisho yote kwenye ukurasa wake wa Instagram mwaka 2024.

Rice, ambaye ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne anayeitwa Jude na Fryer, amesema matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa.

RIC 02

“Kwangu mimi muda ninaotumia kwenye simu si tatizo kubwa. Lakini ninaamini mitandao ya kijamii kwa watoto ni tatizo kwa asilimia 100. Sioni tena ule upekee wa tabia na haiba ambao tulikuwa tunauona miaka michache iliyopita,” amesema.

Wakati akizungumzia maisha yake nje ya uwanja, Rice pia anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na Arsenal, ambao unatajwa kumuingizia mshahara wa takribani pauni 350,000 (Sh bilioni 1.2) kwa wiki.

Mkataba huo utamweka katika kiwango sawa na Bukayo Saka kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi ndani ya klabu hiyo.

Hata hivyo, Rice amesema licha ya utajiri mkubwa unaopatikana katika soka la kisasa, bado anaamini ni muhimu kumfundisha mtoto wake thamani ya fedha na maisha.

RIC 03

“Fedha zinazozunguka kwenye soka ni za ajabu sana. Ni muhimu kuelewa gharama za vitu hata kama huna wasiwasi wa kuvilipia,” amesema.

“Unataka mtoto wako ajue thamani ya maisha na fedha, asilelewe katika mazingira ya kubembelezwa kila kitu. Unataka ajifunze kufanya kazi na kuelewa thamani ya anachopata, usimuache afanye kila anachotaka kwa kuwa unampenda, hapana mpe majukumu hata kama ni mazito atajifunza mambo mengi lakini pia mfundishe kuhusu dunia, hakikisha kila siku anafahamu dunia inaendaje, inatoka wapi, kuna nini kimetokea, kuna nini kitatokea, lakini pia mfundishe kuheshimu wakubwa na wadogo.”

RIC 04

Kwa sasa, Rice anaendelea kuonyesha kiwango bora akiwa na Arsenal, huku kikosi hicho kikiendelea kuwania mafanikio makubwa msimu huu.