Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Refa Dahane akabidhiwa Mamelodi, USM Alger

Muktasari:

  • Mwamuzi wa kimataifa kutoka Mauritania, Dahane Beida, ameteuliwa kuchezesha fainali ya taji la CAF Super Cup 2026 kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na USM Alger ya Algeria. Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Novemba 8, 2026, katika Uwanja wa Loftus Versfeld, jijini Pretoria.

Pretoria, Afrika Kusini. Mwamuzi wa kimataifa kutoka Mauritania, Dahane Beida, ameteuliwa kuchezesha mchezo wa fainali ya taji la CAF Super Cup 2026 kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na USM Alger ya Algeria.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 8, 2026, katika Uwanja wa Loftus Versfeld, jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Mwamuzi huyo aliwahi kusimamia mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022/2023 kati ya USM Alger na Yanga.

Katika mchezo huo uliochezwa jijini Algiers, Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0, lakini USM Alger ikatwaa taji kwa faida ya bao la ugenini, baada ya matokeo ya jumla kuwa sare ya mabao 2-2.

Refa huyo pia alichezesha mechi ya pili ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba na RS Berkane iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.

Beida ni mmoja wa waamuzi wenye uzoefu katika mashindano ya soka barani Afrika. Amewahi kusimamia mechi kubwa za kimataifa, zikiwemo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023 kati ya Ivory Coast na Nigeria.

Mchezo huo unazikutanisha Mamelodi Sundowns, bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, na USM Alger, mshindi wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Fainali hiyo itachezwa kwa mfumo wa mechi moja, ambayo itaamua bingwa wa CAF Super Cup ya mwaka huu.

Fainali ya mwaka huu inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku Mamelodi Sundowns ikilenga kutumia faida ya kucheza nyumbani kutwaa taji hilo, wakati USM Alger ikitaka kuongeza mafanikio yake katika mashindano ya klabu barani Afrika.