Lango la Doumbia lafunguka, aibua vaibu mitaani
Muktasari:
- Bao hilo linahitimisha ukame uliokuwa unamkabili na kuashiria mwanzo mzuri wa safari yake ya kimataifa na klabu hiyo.
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Doumbia, amefungua ukurasa wa mabao baada ya kufunga mawili kwenye mechi dhidi ya 15 de Agosto.
Bao hilo linahitimisha ukame uliokuwa unamkabili na kuashiria mwanzo mzuri wa safari yake ya kimataifa na klabu hiyo.
Doumbia ambaye ametua Simba msimu huu akitokea AS Korofina ya Mali, amekuwa maarufu kutokana na rekodi ya kutofunga kwani awali alikuwa amecheza mechi 11 za mashindano yote bila kutupia nyavuni.
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Doumbia, wakati akifunga bao la kwanza kati ya mawili katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili ya awali dhidi ya 15 de Agosto.
Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akipata sapoti kubwa kutoka kwa benchi la ufundi na mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaamini kuwa bao lake la kwanza la kimataifa dhidi ya !5 de Agosto litamrejeshea ari ya kujiamini na kufungua milango ya mabao katika mashindano inayocheza timu yake.
Mara kadhaa kocha wa kikosi hicho, Steven Barker, amekuwa akizungumza kuhusu mshambuliaji huyo ya kwamba anahitaji muda wa kuvumiliwa, kwani ni mchezaji mzuri.
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Doumbia, wakati akifunga bao la kwanza kati ya mawili katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili ya awali dhidi ya 15 de Agosto.
Baada ya kufunga bao, Doumbia ametoa machozi ya furaha, huku mashabiki na viongozi wakisimama na kumshangilia uwanjani Uhuru, lakini pia shangilia yake iliibua vaibu kubwa kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakifuatilia mchezo huo ndani na nje ya uwanja.