Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford ni kama karusha kijembe hivi

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Staa huyo mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Barcelona kwa mkopo wa msimu mmoja na tangu alipotua kwa miamba hiyo ya Hispania kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, amekuwa panga pangua kwenye kikosi cha kwanza.

BARCELONA, HISPANIA: MARCUS Rashford amefunguka sababu zinazomfanya ang'are huko Barcelona tangu alipoachana na Manchester United.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Barcelona kwa mkopo wa msimu mmoja na tangu alipotua kwa miamba hiyo ya Hispania kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, amekuwa panga pangua kwenye kikosi cha kwanza.

Katika mechi 24 alizocheza msimu huu, Rashford amehusika kwenye mabao 18.

Na kiwango chake kimezidi kunoga zaidi baada ya timu hiyo kurudi uwanjani Nou Camp. Na alipoulizwa kama ataendelea kubaki Hispania hata baada ya msimu huu kumalizika, fowadi huyo wa England amesema: “Bila shaka, hicho ndicho kitu ninachotaka, lakini sio sababu ya mimi kupambana sana. Sababu kubwa ni kwasababu nataka kushinda. Barcelona ni klabu bora.

“Klabu hii inafahamika kwa ushindi, ni aina ya presha ambayo nataka kuwapo si presha mbaya. Nataka presha inayokufanya ufikirie kwenda mbele, presha ya kukuhamasisha kucheza soka.

“Kama klabu haitaki vitu kama hivyo, inakuwa ngumu kuhamasika. Hapa kuna mazingira mazuri yanayofanya nihitaji kuendelea na soka langu.”

Rashford alisifiwa na kocha Hansi Flick mapema mwezi huu, ambaye alisifu kwa kuwa profesheno, aliposema: “Anapokuwa kwenye benchi, hiyo inaonyesha kwamba tuna timu nzuri. Ninachoweza kusema ni mchezaji profesheno, akili yake ni kubwa.“ Barcelona ina ruhusa ya kumsajili jumla Rashford mwishoni mwa msimu.