Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe aweka rekodi mpya Ligi ya Mabingwa Ulaya

MBAPPE Pict

Muktasari:

  • Mbappe alifikisha mechi 100 akiwa na umri wa miaka 27 na siku 298, na kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufikia idadi hiyo, akiipiku rekodi ya Lionel Messi aliyofikisha mechi hizo akiwa na miaka 28 na siku 84.

ROMA, ITALIA: KYLIAN Mbappe ameandika historia mpya katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufikisha mechi 100 katika mashindano hayo na kufunga bao dhidi ya AS Roma, akipanda hadi nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote.

Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alifunga bao lake la 72 katika mashindano hayo, akimpita gwiji wa klabu hiyo, Raul Gonzalez, katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote.

Mbappe alifikisha mechi 100 akiwa na umri wa miaka 27 na siku 298, na kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufikia idadi hiyo, akiipiku rekodi ya Lionel Messi aliyofikisha mechi hizo akiwa na miaka 28 na siku 84.

Mabao 72 ya Mbappe katika Ligi ya Mabingwa yamefungwa akiwa na klabu tatu tofauti. Alifunga mabao sita akiwa Monaco, 42 katika kipindi chake Paris Saint-Germain (PSG) na 24 tangu ajiunge na Real Madrid.

MBAP 01

Ufanisi wake unaonekana zaidi anapolinganishwa na washambuliaji wengine wakubwa katika mechi zao 100 za kwanza kwenye mashindano hayo. Robert Lewandowski alifunga mabao 81 katika mechi zake 100 za mwanzo, huku Messi akifunga 77. Mbappe ana mabao 72, akiwapita washambuliaji wengi maarufu waliowahi kushiriki mashindano hayo.

Hata hivyo, bado ana safari ndefu kufikia vinara wa orodha ya wafungaji bora wa muda wote. Karim Benzema ana mabao 90, Lewandowski 109, Messi 129, huku Cristiano Ronaldo akiongoza kwa mabao 140.

Kwa takwimu hizo, Mbappe anahitaji mabao mengine 18 ili kufikia idadi ya Benzema, ambaye anashika nafasi ya nne katika orodha hiyo. Endapo ataendelea na kiwango chake cha kufunga, mshambuliaji huyo wa Ufaransa ana nafasi ya kupanda zaidi katika orodha hiyo.

MBAP 02

Ronaldo bado ndiye kigezo kikubwa katika mashindano hayo akiwa na mabao 140, hivyo Mbappe anahitaji mabao mengine 68 ili kufikia rekodi hiyo. Pamoja na pengo hilo, umri wake na uwezo wake wa kufunga vinaacha uwezekano wa kuendelea kupanda kwenye orodha hiyo katika misimu ijayo.