Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo mawili yashika mkataba wa Rashford

Muktasari:

  • Barcelona imewekewa kipengele cha kumchukua jumla staa huyo wa England wakati mkataba wake wa mkopo utakapofika tamati mwishoni mwa msimu huu, huku ikitakiwa kulipa Pauni 26 milioni kama ada ya uhamisho ya kumng'oa Manchester United.

BARCELONA, HISPANIA: NDO hivyo. Suala la Barcelona kumbeba jumla Marcus Rashford limedaiwa kuwagawa mabosi wa timu hiyo na hivyo kulifanya jambo hilo kubaki njiapanda.

Barcelona imewekewa kipengele cha kumchukua jumla staa huyo wa England wakati mkataba wake wa mkopo utakapofika tamati mwishoni mwa msimu huu, huku ikitakiwa kulipa Pauni 26 milioni kama ada ya uhamisho ya kumng'oa Manchester United.

Aston Villa yenyewe pia iliwekewa kipengele kama hicho cha kumbeba jumla Rashford wakati alipokuwa kwenye kikosi chao kwa mkopo na ilipaswa kulipa ada ya uhamisho ya Pauni 40 milioni. Lakini, Aston Villa chini ya kocha Unai Emery, iliamua kutokifanyia kazi kipengele hicho na hivyo ilimfungulia mlango wa kutokea Rashford msimu ulipofika tamati.

Rashford, 28, ameonekana kuanza vizuri maisha yake huko Barcelona, ambapo kwenye mechi 18 za kwanza alizocheza kwenye michuano yote, amehusika katika mabao 13 akifunga mabao sita na kuasisti saba.

Awali, ilionekana kama Barcelona ingefanyia kazi kipengele cha kumbeba jumla staa huyo, lakini sasa jambo hilo sasa limeibua mjadala mzito huko kwa mabosi na kuanza kuwazia vitu vilevile ambavyo vinawafanya Man United kutaka aondoke.

Ripoti zinadai kwamba kuna wasiwasi juu ya mshahara mkubwa wa Rashford, licha ya kwamba ada yake ya uhamisho ni ndogo ukilinganisha na uzoefu wake. Rashford alishusha mshahara wake kwa asilimia 25 na sasa analipwa 240,000 kwa wiki na Barca inalipa mshahara wote huo kwa kipindi chote cha mkopo atakapokuwa kwenye kikosi chao.

Kuna madai mengine pia kwamba Rashford ana mchango mdogo kwa kusaidia timu kukaba kuanzia juu, kitu ambacho ni lazima kwenye kikosi cha Hansi Flick. Ripoti hiyo ilibainisha kwamba Rashford alisajiliwa na Barca wakimtazama kama chaguo la pili nyuma ya Raphinha.

Man United yenyewe inaamini hilo litapatiwa ufumbuzi na Rashford atabebwa jumla kwani kocha Ruben Amorim ameshamfuta kwenye mipango yake.

Kocha Flick aliwahi kumsifia Rashford kutokana na kiwango chake cha uwanjani, lakini jambo hilo bado halitoi uhakika kwamba atabebwa jumla huko Nou Camp kutokana na mambo mawili, kwanza mshahara wake na pili ni staili yake ya uchezaji, hakabi kuanzia juu.