Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford atoboa siri kurejea kwenye kiwango

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo, 28, alijiunga na Barcelona kwa mkopo wa msimu mmoja dirisha lililopita na tangu atue amekuwa mchezaji tegemeo kikosi cha kwanza.

BARCELONA, HISPANIA: MARCUS Rashford amefichua sababu ya kurejea kwake katika kiwango bora tangu aondoke Manchester United.

Mshambuliaji huyo, 28, alijiunga na Barcelona kwa mkopo wa msimu mmoja dirisha lililopita na tangu atue amekuwa mchezaji tegemeo kikosi cha kwanza.

Katika michezo 24 aliyocheza msimu huu, Rashford amechangia mabao 18 akifunga saba na kutoa asisti 11.

Rashford alisema kiwango chake kizuri kinatokana na kuongezeka kwa kujiamini na motisha kubwa aliyoipata tangu atue Nou Camp.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kubaki Hispania baada ya msimu kumalizika, Rashford alisema: “Bila shaka hilo ndilo ninalotaka, lakini hiyo sio sababu inayofanya nijitume na kufanya kazi kwa bidii. Sababu kuu ya mimi kuonekana bora ni nataka kushinda. Barcelona ni klabu kubwa sana. Ni klabu inayojulikana kwa kushinda na inanipa presha ya kufanya hivyo kila siku. Ni presha unayoitamani na ninayotaka kuwa nayo ninapocheza soka. Kama nikiwa nipo kwenye klabu ambayo haihitaji mambo hayo ya kushinda, inakuwa vigumu kwangu kupata motisha. Haya ni mazingira mazuri sana kwangu kuendelea na safari yangu ya soka.”

Akizungumzia kuhusu kuzoea maisha ya Catalonia, Rashford alisema:”Tangu dakika ya kwanza nilipofika hapa nilipokelewa vizuri. Kwangu mimi, sababu ya kuwa hapa ni kuisaidia timu. Nipo hapa kusaidia kushinda mataji. Mwaka jana walikuwa na msimu mzuri sana, lakini kama ilivyo maishani na katika soka, mambo hubadilika haraka, hivyo tunapaswa kupambana na kufikia mafanikio ya msimu uliopita.”

Mapema mwezi huu, Kocha wa Barca, Hans Flick alimpongeza staa huyo kutokana na ukomavu wake na jinsi alivyopambana kuhakikisha anaingia katika kikosi haraka iwezekavyo licha ya changamoto mbalimbali.

“Mwanzoni alihitaji muda kidogo kuzoea, lakini sasa yuko kwenye kiwango chake bora,” alisema Flick.

Barcelona ina chaguo la kumsajili mshambuliaji huyo moja kwa moja katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi  baada ya mkopo wake kumalizika.