Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford: Msitaje jina langu kila siku

Muktasari:

  • Rashford alitoa kauli hiyo kupitia mtandao wa X baada ya kujibu kipande cha podikasti ya Stick to Football, ambapo Jamie Carragher alionekana kukerwa baada ya Neville kutaka kusikia maoni kuhusu mshambuliaji huyo.

MANCHESTER, England. MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Marcus Rashford amesema anatamani kucheza soka bila jina lake kutajwa kila siku, baada ya beki wa zamani wa klabu hiyo, Gary Neville, kuanzisha mjadala kuhusu mustakabali wake katika podikasti.

Rashford alitoa kauli hiyo kupitia mtandao wa X baada ya kujibu kipande cha podikasti ya Stick to Football, ambapo Jamie Carragher alionekana kukerwa baada ya Neville kutaka kusikia maoni kuhusu mshambuliaji huyo.

Carragher alisema: “Tunaweza kufanya podikasti bila kumtaja Rashford?” huku akionyesha kuchoshwa na mijadala ya mara kwa mara kuhusu nyota huyo.

Akijibu kipande hicho, Rashford aliandika: “Asante, Jamie. Itakuwa vizuri kujikita kwenye soka na kucheza bila jina langu kutajwa kila siku.”

Rashford, 28, anaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kubaki Manchester United msimu huu baada ya msimu uliopita kuitumikia Barcelona kwa mkopo, ambako alifanikiwa kushinda taji la La Liga.

Mchezo wake wa mwisho wa ushindani akiwa na United ulikuwa Desemba 2024 chini ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Ruben Amorim.

Hata hivyo, Rashford anaweza kurejea kwenye kikosi cha United katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Hull utakaochezwa Jumamosi.

Beki wa United, Harry Maguire, amesema anatumaini Rashford ataendelea kubaki Old Trafford, akisisitiza kuwa mshambuliaji huyo ni “mchezaji muhimu” na “tishio” kwa wapinzani.

Maguire alitoa kauli hiyo baada ya United kupoteza kwa mabao 4-2 dhidi ya AC Milan katika mchezo wa kirafiki Jumamosi iliyopita.