Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matatu Simba, agizo la Serikali


MABADILIKO makubwa matatu yatatokea baada ya Simba kuanza kutelekeza agizo lililotolewa jana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) la kuitaka klabu hiyo kuanza kufuata marekebisho ya katiba yake ya mwaka 2018 iliyofanyiwa marekebisho Novemba 30, 2025.


Hatua hiyo ni ishara moshi mweupe ndani ya Simba umeanza kuonekana kipindi hiki ambacho klabu hiyo ipo kwenye mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji.

Ipo hivi; Kwanza ni katika umiliki wa hisa na mali za upande wa klabu ambapo sasa zitakuwa chini ya Baraza la Wadhamini la Klabu hiyo na sio chini ya kampuni kama ilivyokuwa hapo awali.

Katiba ya mwanzo, ililazimisha hisa za Simba kuwa chini ya Simba Sports Club Holding Company Limited ambayo kwa katiba iliyofanyiwa mabadiliko, chombo hicho kwa sasa hakipo.

Jambo lingine kubwa linalopaswa kutokea ni ukomo wa Bodi ya Wakurugenzi inayosimamia shughuli za Simba hivi sasa kwa vile muundo wake ni kinyume na katiba ya sasa.

Kupoteza uhalali kwa Bodi ya sasa ya Wakurugenzi ya Simba kunatokana na kuundwa kwake na wajumbe kutoka kwa mwekezaji mmoja badala ya wawekezaji watatu kama katiba ya sasa inavyofafanua.

“Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, itamaanisha viongozi waliochaguliwa na kuteuliwa kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya Katiba hii na watakaoteulwa na wawekezaji,” ilifafanua sehemu ya tafsiri ya katiba ya sasa ya Simba.

Badiliko la tatu ni hilo la Simba kuanza kuwa na wawekezaji wasiopungua watatu katika umiliki wa hisa zake asilimia 49 tofauti na hapo awali ambapo mwekezaji alikuwa ni mmoja tu.

Jana, Katibu Mkuu wa BMT, Neema Msitha, alitoa taarifa ya kuitaka Simba kuanza utekelezaji wa katiba hiyo ambayo ilipitishwa Februari 18, 2026.

“Hivyo, Serikali inatoa wito kwa Klabu ya Simba kutumia vyombo na taratibu zake halali kukamilisha utekelezaji wa Katiba iliyoidhinishwa, na kuwasilisha rasmi kwa mamlaka husika masuala yoyote yanayohitaji ufafanuzi.

“Serikali itaendelea kutekeleza jukumu lake la kuendeleza sekta ya michezo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, huku ikilenga maendeleo ya klabu na sekta ya michezo kwa ujumla wake.

“Ni matarajio ya Serikali kuwa masuala ya maendeleo ya michezo yataendelea kushughulikiwa kwa kuzingatia utulivu, uwazi, uwajibikaji na maslahi ya wananchi na wapenzi wa michezo,” alifafanua Msitha.

Msitha alisema wapo tayari kuipokea Simba iwapo kutakuwa na uhitaji wa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa hilo.

“Kwa msingi huo, Serikali inafafanua kuwa ilikamilisha wajibu wake wa kuidhinisha na kukabıdhi Katiba hiyo. Kuanzia hapo, wajibu wa kutekeleza Katiba na kukamilisha mabadiliko yaliyopitishwa na wanachama ni wa Klabu ya Simba yenyewe.

“Utekelezaji wa uamuzi yaliyomo katika Katiba hiyo haupaswi kufanywa na Serikali kwa niaba ya Klabu, kwa kuwa ni uamuzi yaliyofanywa na wanachama kupitia Mkutano Mkuu na kuidhinishwa kwa mujibu wa sheria.

“Hata hivyo, Serikali inatambua kuwa utekelezaji wa mabadiliko hayo unaweza kuibua masuala ya utaratibu unaohitaji ufafanuzi. Kwa hiyo, BMT na taasisi nyingine husika za Serikali ziko tayari kuipokea Klabu ya Simba kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa utaratibu pale inapohitajika, kwa mujibu wa mamlaka ya kila taasisi,” imefafanua BMT.