Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raphinha wa moto kinoma La Liga

RAPHINHA Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa Brazil alionyesha ubora mkubwa wa kumalizia nafasi, akifikisha mabao 14 katika mashindano yote msimu huu.

SEVILLA, HISPANIA: MSHAMBULIAJI Raphinha alifunga hat-trick yake ya pili mfululizo na kuiongoza Barcelona kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Sevilla kwenye Uwanja wa Ramon Sanchez-Pizjuan, matokeo yaliyoifanya timu hiyo kuongeza uongozi wake kileleni mwa La Liga.

Mshambuliaji huyo wa Brazil alionyesha ubora mkubwa wa kumalizia nafasi, akifikisha mabao 14 katika mashindano yote msimu huu.

Raphinha pia alifunga mabao matatu katika ushindi wa Barcelona wa 7-2 dhidi ya Racing Santander Jumatano iliyopita.

RAPHI 01

Ushindi huo umeifanya Barcelona kufikisha pointi 21, ikiwa na pengo la pointi sita dhidi ya Real Madrid iliyo nafasi ya pili na Real Betis iliyo nafasi ya tatu. Hata hivyo, Barcelona imecheza mchezo mmoja zaidi.

Sevilla ilianza mchezo kwa kufunga bao la kwanza dakika ya 19, baada ya shambulizi lililoandaliwa vizuri kumalizika kwa Felix Correia kupiga krosi ya chini kuelekea langoni, ambako Youssouf Fofana aliunganisha kwa kichwa na kuandika bao hilo.

RAPHI 02

Lakini Raphinha aliisawazishia Barcelona dakika tatu baadaye, alipokatiza kuelekea ndani na kupiga shuti la utulivu lililompita kipa wa Sevilla, Odysseas Vlachodimos.

Kijana Lamine Yamal alikuwa mhimili wa bao la pili la Raphinha dakika ya 52, baada ya kumzidi ujanja beki kwa kupiga chenga kuelekea nje ya lango kabla ya kupiga krosi iliyomkuta Mbrazil huyo, aliyefunga kwa kichwa.

RAPHI 03

Yamal alitoa pasi nyingine muhimu dakika ya 69, alipompenyezea Raphinha mpira kwa ustadi mkubwa, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akimpiga kipa Vlachodimos mpira wa juu kwa ustadi na kuufanya uingie wavuni.

Bao hilo lilifunga ushindi wa saba mfululizo wa Barcelona katika La Liga na wa nane katika mashindano yote.

Sevilla, kwa upande wake, iliendelea kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 13.