Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ndo siri Shakira kuonekana ‘mtoto’

Muktasari:

  • Akiwa ametimiza miaka 49, mwonekano wake bado unaendelea kuwavutia mashabiki duniani kutokana na ngozi yake yenye mng’aro, uso wenye afya na mwonekano unaomfanya aonekane mwenye nguvu na uchangamfu.

KUMEKUWA na mijadala mingi mtandaoni kuhusu umri wa mwanamuziki nyota wa Colombia, Shakira na namna anavyoonekana kuwa kama motto wa 2000.

Akiwa ametimiza miaka 49, mwonekano wake bado unaendelea kuwavutia mashabiki duniani kutokana na ngozi yake yenye mng’aro, uso wenye afya na mwonekano unaomfanya aonekane mwenye nguvu na uchangamfu.

Shakira, ambaye amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miongo miwili ni miongoni mwa wasanii wanaozingatia afya na mwonekano wao.

Siri hiyo inatokana na mazoezi, lishe, mapumziko, utunzaji wa ngozi pamoja na matumizi ya baadhi ya vifaa vinavyosaidia kuboresha mwonekano wa uso.

Kwenye moja ya mahojiano Shakira aliwahi kusema: “Zamani nilikuwa nakula kila kitu bila kufanya mazoezi niliongezeka kilo sana kwa hiyo nikawa nawekewa ratiba ya mazoezi na aina ya vyakula.”

Sasa wengi wamekuwa wakijiuliza nini siri ya urembo wa mpenzi huyo wa zamani wa nyota wa Barcelona, Gerald Pique. Kuna baadhi ya video zimekuwa  zikimuonyesha Shakira akiwa kwenye maandalizi ya shoo zake lazima atumie kifaa ambacho huwa anajisugulia usoni.

Kifaa hicho kinaitwa  Lymphatic drainage facial massage ni aina ya masaji inayolenga kusaidia kupunguza mkusanyiko wa maji kwenye tishu za uso na kuufanya uso uonekane wenye mwonekano uliochangamka zaidi.

Kifaa hicho hakifanyi miujiza wala hakirudishi umri nyuma kama ambavyo baadhi ya watu wanaweza kudhani. Badala yake, hutumika kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kutunza ngozi. Wataalamu wa ngozi wanaeleza mbinu za aina hiyo zinaweza kusaidia kupunguza uvimbe wa muda kwenye uso na kuufanya mwonekano wa ngozi uwe mzuri zaidi.

Moja ya sababu zinazofanya kifaa hicho kuvutia ni uwezo wake wa kusaidia kupunguza uvimbe mdogo wa uso, hasa baada ya kuamka asubuhi. Hali hiyo inaweza pia kujitokeza baada ya safari ndefu, uchovu au mabadiliko ya ratiba ya usingizi.

Kwa mtu kama Shakira ambaye mara kwa mara anakuwa kwenye kamera, jukwaani au katika matukio mbalimbali ya kimataifa, mwonekano wa uso ni sehemu muhimu ya kazi yake.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Mbali na kupunguza uvimbe wa muda, masaji ya uso inaweza kuchochea mzunguko wa damu katika eneo linalofanyiwa masaji. Hali hiyo inaweza kufanya ngozi ionekane yenye afya na mng’aro zaidi kwa muda. Hata hivyo, matokeo yanaweza kutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine.

Jambo lingine linalovutia ni namna masaji ya aina hiyo inavyoweza kufanya mstari wa taya na mashavu kuonekana vizuri zaidi kwa muda kutokana na kupungua kwa uvimbe wa uso. Ndiyo maana wakati mwingine watu wanaweza kuona tofauti katika mwonekano wa uso kabla na baada ya kutumia mbinu hizo.

Katika utaratibu wa kutunza ngozi, kifaa hicho pia kinaweza kutumika pamoja na bidhaa mbalimbali kama vile serum na moisturizer.

Hata hivyo wataalamu wanaeleza ni muhimu kutumia bidhaa zinazofaa aina ya ngozi na kufuata maelekezo ya matumizi ili kuepuka kuwasha au kuharibu ngozi.

Siyo Shakira pekee anayetumia kifaa hicho baadhi ya wasanii duniani wamekuwa wakifanya hivyo lengo kupata muonekano wa tofauti na kuwa bora siku zote. Miongoni mwao ni Beyonce.

Mwonekano wa ngozi huathiriwa na mambo mengi, ikiwemo lishe, usingizi, mazoezi, mazingira na namna mtu anavyotunza ngozi yake kwa muda mrefu. Kwa Shakira, mazoezi yamekuwa sehemu muhimu ya maisha yake.

Mwanamuziki huyo amekuwa akijulikana kwa kujishughulisha na mazoezi mbalimbali yanayomsaidia kuwa tayari kwa mahitaji ya jukwaa.

Kwa msanii anayefanya maonyesho yenye nguvu na kucheza kwa muda mrefu, kuwa na mwili wenye uwezo wa kuhimili shughuli hizo ni muhimu.

Lishe pia ni sehemu nyingine inayoweza kuchangia afya kwa ujumla. Kula mlo wenye uwiano, kunywa maji ya kutosha na kupata virutubisho vinavyohitajika na mwili ni mambo yanayoweza kusaidia afya ya ngozi pamoja na afya kwa ujumla.

Jambo jingine muhimu ni matumizi ya sunscreen. Mionzi ya jua inaweza kuathiri ngozi kwa muda mrefu, hivyo wataalamu wa ngozi mara nyingi husisitiza matumizi ya kinga dhidi ya miale ya jua kama sehemu ya utaratibu wa kila siku wa kutunza ngozi. Sasa hivo ndivyo vitu anavyofanya Shakira na kuonekana mwenye mvuto kila siku.