Australia haiitishwi na Argentina, Denmark
Muktasari:
- Australia ipo Kundi C pamoja na Argentina, Denmark na Msumbiji, ambapo ilianza kampeni yake kwa kuvaana na Argentina Novemba 19, kabla ya kukutana na Denmark Novemba 22 na kumalizia hatua ya makundi dhidi ya Msumbiji Novemba 25.
Kocha mkuu wa Australia, Carl Veart, amesema kikosi chake hakina wasiwasi wala kuiogopa timu yoyote katika Fainali za Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17 (U-17) Qatar 2026.
Kocha huyo alisisitiza kuwa timu hiyo inakwenda kuonyesha uwezo wake na ubora wa soka la nchi hiyo licha ya kukutana na wapinzani wenye uzoefu tofauti katika mashindano hayo.
Australia ipo Kundi C pamoja na Argentina, Denmark na Msumbiji, ambapo ilianza kampeni yake kwa kuvaana na Argentina Novemba 19, kabla ya kukutana na Denmark Novemba 22 na kumalizia hatua ya makundi dhidi ya Msumbiji Novemba 25.
Veart amesema anatambua ushindani uliopo, lakini kikosi hicho kinajiamini na kina dhamira ya kuonyesha inahitaji kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa.
“Tunatambua kuwa tutakutana na timu bora dhidi ya timu bora, lakini sidhani kama tunapaswa kuiogopa timu yoyote,” amesema Veart.
“Badala yake, tutaingia katika michezo hiyo tukiwa na kujiamini na dhamira ya kuonyesha uwezo wetu pamoja na kile ambacho soka la Australia linawakilisha.”
Miongoni mwa nyota wanaounda kikosi hicho wanatoka ligi ya nje. Wachezaji hao ni Charlie Wilson-Papps wa Brighton, Jariyah Shaw wa Manchester United, Max Lyall-Rajendra wa AFC Bournemouth na Harrison Bond wa Red Bull Salzburg.
Argentina ndiyo timu inayoonekana kuwa na ushindani mkubwa katika kundi hilo, ikiwa na historia kubwa ya kushiriki mashindano hayo, ingawa haijawahi kutwaa ubingwa.
Imeshiriki mara 16 kati ya 20 ya Kombe la Dunia U-17 na kumaliza nafasi ya tatu mara tatu, lakini katika mashindano yalilopita ilitolewa hatua ya 32 bora.
Tofauti na Argentina, Denmark inashiriki kwa mara ya pili, wakati Msumbiji ikiweka historia ya kuwa taifa la kwanza kutoka nchini humo kushiriki mashindano hayo.
Mbali na matokeo, Australia pia ina dhamira ya kutumia mashindano hayo kuhamasisha kizazi kijacho cha wachezaji nchini humo.