Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

POGBACK: Kibonzo cha Pogba cha Man United chashtua mashabiki

Muktasari:

  • Supastaa huyo wa Les Bleus aliposti kibonzo kwenye ukurasa wake wa Instagram kikifichua uwezekano wa kurejea katika kikosi cha Man United chenye maskani yake Old Trafford.

MANCHESTER, ENGLAND: ETI arudi, asirudi? Swali konki kwa mashabiki wa Manchester United juu ya kiungo wao wa zamani fundi wa boli, Paul Pogba.

Supastaa huyo wa Les Bleus aliposti kibonzo kwenye ukurasa wake wa Instagram kikifichua uwezekano wa kurejea katika kikosi cha Man United chenye maskani yake Old Trafford.

Pogba, 31, kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kusitisha mkataba huko Juventus kwa makubaliano ya pande mbili, hivyo ana ruhusa ya kuachana na miamba hiyo ya Serie A.

Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa ni ruhusa kucheza kuanzia Machi mwaka huu baada ya adhabu ya kufungiwa kupunguzwa hadi miezi 18.

Pogba mwanzoni alifungiwa kucheza soka kwa miaka minne na NAO Italia kufuatia kupimwa na kupata majibu juu ya virutubisho vya DHEA vilivyopigwa marufuku michezoni kutokana na kusisimua misuli. Hata hivyo, wakati adhabu yake ikiwa imepunguzwa kutoka miaka minne hadi miezi 18, kiungo huyo kwa sasa anatafuta timu nyingine ya kuendelea na soka lake baada ya Juventus kuachana naye.

Na dirisha la usajili wa majira ya baridi huko Ulaya likiwa wazi hadi Februari 3, supastaa huyo anatafuta timu ambayo ataanza kuitumikia kuanzia Machi wakati adhabu yake itakapofika ukomo.

Football Insider iliwahi kufichua huko nyuma kwamba mpango wa kurudi kwenye Ligi Kuu England haukuwepo kwenye mfumo kutokana na kwamba hakuna klabu inahitaji saini yake, lakini sasa Pogba ametuma meseji ya kushtua kama vile anataka jambo hilo litokee arudi kukipiga kwenye ligi anayoifahamu vyema.

Na sasa Pogba ameibua minong’ono ya kurejea Old Trafford baada ya kuposti picha ya kibonzo kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambapo alijichora yeye pamoja na Amad Diallo wakiwa wamesimama ndani ya uzi wa Man United.

Picha hiyo ya kibonzo ilikwenda sambamba na maneno aliyoandika, “Acha tusubiri tuone nini kinakuja …”

Jambo hilo liliwaibua mashabiki wa Man United na kuweka komenti zao juu ya ishu ya Pogba kurudi kukipiga kwenye kikosi cha Man United, ambayo kwa sasa ina viungo kadhaa akiwamo Manuel Ugarte, Bruno Fernandes, Christian Eriksen, Kobbie Mainoo, Casemiro na kinda anayeibukia kwa kasi Toby Collyer.

Pogba anaamini atakwenda kuuwasha moto akicheza sambamba na Amad kwenye fomesheni ya 3-4-2-1 inayotumiwa na kocha Mreno Ruben Amorim ambaye bado anajitafuta kwenye kikosi hicho.

Shabiki wa kwanza aliandika kwenye X: “Yeye na Amad kwenye ile Namba 10.”

Shabiki wa pili alitwiti: “Tunamhitaji hata kwa miezi sita sitajali.”

Shabiki wa tatu alihoji: “Hapana, hatumhitaji Pogba, amekwisha.”

Na shabiki wa nne alikomenti: “Pogba wa bure sio mbaya.”

Shabiki wa tano alisema: “Ile Pogba-Amad-Mazrizzy muunganiko wa maana kucheza kwenye upande wa kulia.”

Pogba aliwahi kukipiga kwenye kikosi cha Man United, alipotamba na timu hiyo kwa awamu mbili tofauti baada ya kuibukia kutoka kwenye akademia ya miamba hiyo ya Old Trafford.

Alicheza mechi saba tu kwenye awamu yake ya kwanza kabla ya kuondoka kwenda Juventus na kisha kurudi tena Old Trafford kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2016.

Kiungo huyo alirudi Man United akitokea Juventus kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia kwa wakati huo - Pauni 89.3 milioni.

Lakini ilipofika majira ya kiangazi 2022, Pogba aliondoka Man United kwenda kujiunga na Juventus kwa uhamisho wa bure kabisa baada ya mkataba wake huko Old Trafford kufika ukomo.

Kwenye awamu ya pili Juventus, mambo hayakuwa mazuri kabisa kwa Pogba, ambapo alikabiliwa na majeraha ya muda mrefu kabla ya kukutwa na janga la kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni kutokana na kuwa na virutubisho vya kusisimua misuli.

Kwenye Ligi Kuu England, Pogba alicheza mechi 157, akifunga mabao 29 na kuasisti mara 38. Na sasa anapatikana bure kabisa, huku akiwa na ruhusa ya kucheza tena kuanzia Machi mwaka huu.