Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubingwa England kaa la moto

UBINGWA Pict

Muktasari:

  • Baada ya miaka ya utawala wa Manchester City chini ya Pep Guardiola, kisha Liverpool na Arsenal kutwaa ubingwa kwa tofauti ya angalau pointi saba, safari hii mazingira yanaashiria vita vya wazi vya ubingwa vinavyoweza kuhusisha klabu nyingi.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England imezoeleka kuwa na mabingwa wanaotawala kwa muda mrefu, lakini msimu wa 2026-27 unaonekana kuvunja utamaduni huo.

Mabadiliko ya makocha, majeraha ya nyota muhimu na matumizi makubwa ya fedha kwenye usajili vimefungua milango ya mbio za ubingwa ambazo zinaweza kuwa ngumu zaidi kutabiri kuliko ilivyowahi kutokea katika miaka ya karibuni.

Baada ya miaka ya utawala wa Manchester City chini ya Pep Guardiola, kisha Liverpool na Arsenal kutwaa ubingwa kwa tofauti ya angalau pointi saba, safari hii mazingira yanaashiria vita vya wazi vya ubingwa vinavyoweza kuhusisha klabu nyingi.

UBING 04
UBING 04

Makocha wapya, ushindani mpya

Kwa mara ya kwanza baada ya muongo mmoja, Manchester City itaingia kwenye msimu bila kocha wake aliyewapa mafanikio makubwa, Pep Guardiola.

Guardiola, aliyeshinda mataji 17 makubwa ndani ya miaka 10 akiwa Etihad, ameondoka na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa msaidizi wake, Enzo Maresca.

Chelsea nayo imeanza ukurasa mpya baada ya kumteua Xabi Alonso kuwa kocha mkuu. Alonso, ambaye aliandika historia kwa kuipa Bayer Leverkusen ubingwa wa Bundesliga bila kupoteza mechi, anarejea England baada ya kipindi kisichokuwa rahisi akiwa Real Madrid.

Liverpool pia imechagua mwelekeo mpya kwa kumteua Andoni Iraola kufuatia kuondoka kwa Arne Slot, huku Manchester United na Tottenham nazo zikiwa chini ya Michael Carrick na Roberto De Zerbi, ambao walichukua timu hizo katikati ya msimu uliopita.

Hivyo, kati ya vigogo sita wa jadi wa England, ni Mikel Arteta wa Arsenal pekee aliyebaki kwenye nafasi yake tangu msimu uliopita.

UBING 01

Saliba aipa Arsenal presha

Arsenal, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu wameanza kwa pigo kabla hata ya msimu kuanza baada ya beki tegemeo William Saliba kupata majeraha ya mgongo akiwa kwenye Kombe la Dunia na Ufaransa.

Saliba alicheza mechi 50 katika mashindano yote msimu uliopita na ushirikiano wake na Gabriel uliifanya Arsenal kuwa timu iliyofungwa mabao machache zaidi kwenye ligi.

Takwimu zinaonyesha tofauti kubwa akiwa uwanjani na akiwa nje. Tangu aanze kuichezea Arsenal mwaka 2022, timu hiyo imeshinda asilimia 68.7 ya mechi zake za Premier League akiwa kikosini, lakini kiwango hicho hushuka hadi asilimia 47.6 anapokosekana.

Jambo hilo linaweza kuwa changamoto kubwa kwa Arsenal ambayo inaanza msimu kwa ratiba ngumu ikiwakabili Aston Villa na Chelsea katika mechi mbili kati ya tatu za mwanzo.

UBING 02

Ratiba ya Ulaya inaweza kuitesa United?

Manchester United ilifaidika kwa kutokuwa na mechi nyingi msimu uliopita, ikicheza jumla ya michezo 40 pekee katika mashindano yote na kumaliza nafasi ya tatu.

Kwa upande mwingine, Chelsea ilicheza mechi 59 na kumaliza nafasi ya 10, huku Tottenham ikicheza 52 na kunusurika kushuka daraja katika siku ya mwisho wa msimu.

Msimu huu hali imebadilika. United na klabu nyingine nane za England zitakuwa na majukumu ya mashindano ya Ulaya, wakati Chelsea na Tottenham hazitashiriki michuano hiyo.

Ili kuongeza nguvu kikosini, United tayari imesajili viungo Andrey Santos na Youri Tielemans, lakini bado kuna maswali kama kikosi hicho kitakuwa na kina cha kutosha kuhimili ratiba ngumu.

UBING 03

Chelsea na Spurs kuwa farasi weusi?

Baada ya misimu ya kusuasua, Chelsea na Tottenham zimeonyesha dhamira kubwa ya kurejea kileleni kupitia usajili.

Chelsea imevunja rekodi kwa kumsajili Morgan Rogers kutoka Aston Villa kwa Pauni 117 milioni, na kumfanya kuwa mchezaji wa Uingereza aliyenunuliwa kwa ada kubwa zaidi kuwahi kutokea.

Mbali na Rogers, imeongeza Marco Palestra kwa Pauni47 milioni, huku mazungumzo yakiendelea kuwasajili Danny Welbeck, Jordan Henderson na Maxence Lacroix.

Kwa upande wa Tottenham, matumizi yao yamefikia karibu Pauni 237 milioni, yakiweka rekodi mpya ya klabu.

Spurs walivunja rekodi yao ya usajili mara mbili ndani ya siku mbili baada ya kuwasajili Mateus Fernandes kwa Pauni milioni 85 na Sandro Tonali kwa Pauni milioni 100. Pia wameongeza Jan Paul van Hecke, Marcos Senesi, Andrew Robertson na Martin Dubravka.

Kwa mabadiliko makubwa ya makocha, usajili wa wachezaji wapya na changamoto za ratiba, msimu wa 2026-27 unaonekana kuwa mmoja wa misimu migumu zaidi kutabiri bingwa wa Ligi Kuu England.