Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pereira aweka rekodi WAFCON

PEREIRA Pict

Muktasari:

  • Pereira alifunga bao hilo Agosti 2, 2026, dhidi ya Mali katika kichapo cha mabao 3-2 akifanya hivyo dakika ya 36, tukio alilolielezea ni zaidi ya mafanikio yake binafsi kutokana na namna lilivyowakilisha safari mpya ya soka la wanawake nchini humo.

MSHAMBULIAJI wa Cape Verde, Eveline Pereira amesema bao alilofunga kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026, limebeba maana kubwa kwake na kwa taifa lake, akiandika historia ya kufunga bao la kwanza kwa nchi yake katika mashindano hayo.

Pereira alifunga bao hilo Agosti 2, 2026, dhidi ya Mali katika kichapo cha mabao 3-2 akifanya hivyo dakika ya 36, tukio alilolielezea ni zaidi ya mafanikio yake binafsi kutokana na namna lilivyowakilisha safari mpya ya soka la wanawake nchini humo.

Akizungumzia bao hilo, Pereira amesema “Ilikuwa hisia ambayo ni ngumu kuielezea. Ilikuwa zaidi ya bao. Ilikuwa wakati wa kihistoria kwangu na kwa Cape Verde. Kujua wakati huu umewahamasisha watu wengi kunaufanya moyo wangu ufurike.”

PERE 01

Mchezaji huyo amesema baada ya tukio hilo alipokea jumbe nyingi za pongezi, fahari na moyo kutoka kwa wananchi wa Cape Verde, huku akieleza jambo kubwa kwake lilikuwa kuona mafanikio hayo yakiwafanya watu wengi wajione sehemu ya historia hiyo.

“Nilipokea upendo mkubwa, maneno ya fahari na moyo. Jambo zuri zaidi lilikuwa kutambua watu wengi walijiona kupitia mimi. Hilo lina thamani kubwa zaidi kuliko takwimu yoyote,” amesema Pereira.

PERE 02

Pereira, ambaye anacheza soka la kulipwa Ureno, amesema anabeba fahari ya kuiwakilisha Cape Verde pamoja na kumbukumbu za hisia alizopitia WAFCON, akisisitiza mafanikio yake yanaweza kuwa mwanzo wa njia kwa wasichana wengine wanaotamani kucheza soka.

“Ninachokwenda nacho ni fahari ya kuiwakilisha nchi yangu, hisia nilizopitia na uhakika kwa kufanya kazi na kuwa mvumilivu, inawezekana kufungua njia kwa wanamichezo wengine. Hili litabaki milele,” amesema.

Cape Verde ambayo iliyoshiriki WAFCON kwa mara ya kwanza, iliandika historia ya kukusanya pointi moja katika mashindano hayo baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Cameroon, timu hiyo ilimaliza mkiani na pointi moja kwenye kundi D.