Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pedro alianza na Carolina, anastaafu na Patricia!

Muktasari:

  • Pedro, mshindi wa Kombe la Dunia 2010 akiwa na timu ya taifa ya Hispania, ametangaza uamuzi huo akiwa na umri wa miaka 39. Mzaliwa huyo wa visiwa vya Canary, alikuwa hana timu tangu alipoondoka Lazio ya Italia Juni 30 mwaka huu.

KATI ya waliompongeza staa wa zamani wa Barcelona na Chelsea, Pedro Rodriguez baada ya kutangaza kustaafu soka wiki iliyopita, ni pamoja na aliyekuwa mke wake, Carolina Martin ambaye walijaliwa kupata watoto watatu katika ndoa yao.

Pedro, mshindi wa Kombe la Dunia 2010 akiwa na timu ya taifa ya Hispania, ametangaza uamuzi huo akiwa na umri wa miaka 39. Mzaliwa huyo wa visiwa vya Canary, alikuwa hana timu tangu alipoondoka Lazio ya Italia Juni 30 mwaka huu.

"Leo unafunga ukurasa muhimu sana katika maisha yako. Ukurasa uliojaa ndoto, juhudi na nyakati ambazo zitabaki milele katika historia ya soka.

Nimebahatika kushuhudia kwa ukaribu mafanikio yako mengi na kuandamana nawe kwa miaka mingi katika safari iliyohitaji juhudi kubwa sana ndani na nje ya uwanja," aliandika Carolina kupitia Instagram na kuongeza:

"Kutoka moyoni mwangu, nakutakia ukurasa huu mpya wa maisha yako ujae matumaini, changamoto mpya na mafanikio mengi katika kila mradi utakaoamua kuufanyia kazi.”

Ikumbukwe Pedro amestaafu akiwa mchezaji pekee duniani aliyeshinda ubingwa wa UEFA Champions League, Europa League, UEFA Super Cup, Kombe la Dunia la Klabu, EURO na Kombe la Dunia la FIFA.

Pedro na Carolina waliachana mwaka 2017 baada ya vyombo vya habari vya Uingereza kuchapisha picha zilizomuonyesha mchezaji huyo wa Chelsea akimbusu mwanamke mwingine katika mitaa ya London.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya Carolina, tukio hilo lilitokea wakiwa tayari wameachana, hivyo akaomba kwa heshima ya watoto wao hasihusishwe kivyovyote vile na jambo hilo.

"Kutokana na taarifa na uvumi wa hivi karibuni kuhusu uhusiano wangu na Pedro Rodriguez, mchezaji wa Chelsea FC, nimeona ni muhimu kuweka wazi ukweli wa jambo hilo.

"Ndoa yetu ilifikia mwisho miezi kadhaa iliyopita. Tunaomba tuheshimiwe, hasa kwa ajili ya watoto wetu. Namtakia kila la heri katika maisha yake binafsi na ya soka," alieleza Carolina katika taarifa yake.

Kwa mara ya kwanza wawili hao walikutana katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya aliyekuwa mlinda mlango wa Barcelona, Victor Valdes ambaye alikuwa rafiki yao wa karibu.

Kufikia Juni 2015 wakafunga ndoa, kisha miaka miwili baadaye wakajaliwa mtoto wao kwanza aitwaye Bryan.

Familia yao iliongezeka mnamo Agosti 2016 walipopata mtoto wao wa pili, Kyle, na baadaye Julai 2017 walimpata mtoto wao wa tatu, Marc.

Wakati wa ndoa yao, pia walianzisha Taasisi ya Pedro Rodriguez de Lesma, inayolenga kuwasaidia watoto wanaishi katika mazingira magumu katika visiwa vya Canary hasa Tenerife ambako sehemu kubwa ya familia ya Pedro inaishi. Carolina ndiye alikuwa akisimamia shughuli za taasisi hiyo.

Kwa miaka mingi Carolina alikuwa miongoni mwa mashabiki waliohudhuria sana mechi za Pedro alipokuwa akiichezea Barcelona. Pia ni rafiki wa karibu wa mke wa kiungo wa zamani wa Chelsea, Cesc Fabregas, Daniella Semaan. Hivyo kuachana kwa Pedro na Carolina kulijulikana na wengi baada ya picha za mchezaji huyo akiwa na mwanamke mwingine kusambaa kwenye magazeti ya udaku nchini Uingereza. Mwanamke huyo ni Patricia Magaaa ambaye kwa sasa ndiye mpenzi wake!.

Pedro na Patricia tayari wana mtoto mmoja aitwaye Adriana ambaye ana umri wa miaka miwili. Wawili hao kupitia mitandao ya kijamii wameonyesha kupendana sana ambapo mchezaji huyo kila mara amekuwa akiposti picha akiwa na Patricia.

Katika siku ya kuzaliwa ya Patricia mwaka uliopita ambapo alikuwa akisheherekea kutimiza umri wa miaka 33, Pedro aliandika ujumbe ufuatao Instagram akimtakia heri ya kuzaliwa.

"Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu!. Natumaini utafurahia sana siku hii maalumu. Wewe ni mama wa kipekee sana na mwanamke wa shoka. Adriana na mimi tuna bahati kubwa kuwa nawe katika maisha yetu.

"Ninajivunia sana wewe kwa moyo wangu wote. Tuendelee kufurahia pamoja nyakati nyingi nzuri za kifamilia yetu. Nakupenda!," aliandika Pedro.

Kwa mujibu wa picha zao mtandaoni, Patricia anaishi vizuri na watoto wa Perdo na Patricia akiwa kama mama wa kambo. Hata hivyo, haijajulikana iwapo watoto wa Patricia wanaishi nyumba moja na baba yao au huenda kumsalimia kwa vipindi fulani.

Ikumbukwe mafanikio makubwa Pedro katika soka aliyapata akiwa Barcelona ambapo alishinda mataji matano ya Ligi Kuu Hispania (La Liga), matatu ya UEFA, matatu ya Copa del Rey, matatu ya UEFA Super Cup na mawili ya Kombe la Dunia la Klabu.