Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick: ishu ya Martinez imefungwa

Muktasari:

  • Martinez, mwenye umri wa miaka 28, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha United kitakachovaana na Leeds United katika Uwanja wa Elland Road, leo, baada ya kuomba radhi kwa kuwakosoa mkurugenzi wa masuala ya soka, Jason Wilcox, pamoja na viongozi wengine wa klabu hiyo.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesisitiza kuwa sakata la beki Lisandro Martinez halitavuruga mipango ya timu hiyo ya kurejesha makali yake baada ya matokeo yasiyoridhisha katika michezo ya hivi karibuni.

Martinez, mwenye umri wa miaka 28, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha United kitakachovaana na Leeds United katika Uwanja wa Elland Road, leo, baada ya kuomba radhi kwa kuwakosoa mkurugenzi wa masuala ya soka, Jason Wilcox, pamoja na viongozi wengine wa klabu hiyo.

Kauli hizo zilimwingiza kwenye matatizo beki huyo wa Argentina, ambaye pia alitozwa faini na klabu kufuatia mahojiano yake ya televisheni yaliyosababisha mjadala mkubwa ndani na nje ya Manchester United.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Carrick alisema hakuna jambo kubwa lililotokea kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhani, akisisitiza kuwa pande zote zimeelewana na suala hilo limefungwa.

“Watu wanataka kusikia habari kubwa kuhusu mazungumzo makubwa, lakini kwa kweli ilikuwa jambo rahisi. Sote tulielewa hali ilivyokuwa na maana yake.

“Lisandro alitoa kauli yake na kukiri kuwa alifanya kosa. Kwetu sisi kama kundi, hili si jambo la kutengeneza drama. Kwa kweli, tumeshalisahau na kusonga mbele,”€  alisema Carrick.

Kocha huyo alifafanua kuwa kitendo cha Martinez kukubali makosa yake na kutoa tamko la kuomba radhi kimetosha kwa klabu kuendelea na shughuli zake bila kuangalia nyuma.

Kauli za Martinez zilikuwa zimeibua hofu ya kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo vya United, hasa baada ya nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Wayne Rooney, kuonya kuwa ukosoaji wa beki huyo kuhusu sera ya usajili unaweza kusababisha ufa ndani ya kikosi.

Hata hivyo, Carrick amepinga hofu hiyo, akisema hali ya wachezaji mazoezini inaonyesha kuwa kikosi bado kiko imara na kina ari ya kupambana kubadili mwenendo wa matokeo.

“Leo kikosi kilikuwa katika hali nzuri sana, bora zaidi kuliko nilivyokiona kwa muda fulani. Tunaishi hali hii kila siku na tunajua tunavyojisikia.

“Sisi ni watu wenye hisia, shauku na tunajali sana. Wakati mwingine mtu anaweza kusema jambo ambalo hakupaswa kulisema kwa wakati huo, lakini hilo halituzuii kuendelea kujenga mazingira mazuri na mshikamano ndani ya timu,”  alisema.

Carrick aliongeza kuwa licha ya matokeo ya hivi karibuni kutokuwa mazuri, mazoezi ya timu yameonyesha dalili za wazi za wachezaji kutaka kubadilisha hali ilivyo.

Kwa mujibu wa kocha huyo, kipindi cha siku mbili za mazoezi kimekuwa na hali nzuri, huku wachezaji wakionyesha dhamira ya kuibeba timu kutoka kwenye wakati mgumu inayopitia.

Alisema wakati mwingine matukio yenye utata yanaweza kuimarisha mshikamano wa kikosi badala ya kukivunja, na anaamini sakata la wiki hii limekuwa na matokeo hayo kwa Manchester United.

Mbali na Martinez, Carrick pia alizungumzia ujumbe wa hasira uliowekwa mitandaoni na winga Amad Diallo usiku wa Jumanne baada ya mchezo wa timu hiyo.

Amad alionyesha kukerwa na matokeo kwa kuandika ujumbe uliokuwa na lugha kali, akieleza kuwa hakuwa na maneno ya kuelezea kilichotokea.

Carrick alisema ujumbe huo unaonyesha namna wachezaji wanavyojali klabu yao, lakini akasisitiza umuhimu wa kuelekeza hisia hizo kwa njia sahihi.

“Kwa upande mmoja, inaonyesha kuwa wachezaji wanajali sana. Lakini kuna namna ya kufanya mambo na ni sehemu ya kujifunza.”