Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta aunga mkono ajira 60 kufutwa Arsenal

Muktasari:

  • Arsenal imepanga kufanya mabadiliko hayo katika idara mbalimbali zisizohusika moja kwa moja na shughuli za uwanjani. Hata hivyo, wafanyakazi wa benchi la ufundi la timu za wanaume na wanawake, kitengo cha shughuli za kijamii, taasisi ya Arsenal Foundation pamoja na walinzi hawataathirika na mpango huo.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, ametetea uamuzi wa klabu hiyo kupunguza wafanyakazi 60, akisema hatua hiyo inalenga kuweka watu katika nafasi sahihi na kuwekeza zaidi ili kufanikisha malengo ya klabu.

Arsenal imepanga kufanya mabadiliko hayo katika idara mbalimbali zisizohusika moja kwa moja na shughuli za uwanjani. Hata hivyo, wafanyakazi wa benchi la ufundi la timu za wanaume na wanawake, kitengo cha shughuli za kijamii, taasisi ya Arsenal Foundation pamoja na walinzi hawataathirika na mpango huo.

Uamuzi huo umekuja wiki moja tu baada ya Arsenal kutangaza kumuongezea mkataba Arteta wa miaka minne, unaoripotiwa kuwa na thamani ya pauni 20 milioni kwa mwaka.

Akizungumzia mpango huo, Arteta alisema suala hilo limefanyiwa uchambuzi ndani ya klabu, lakini hakujiona kuwa mtu sahihi wa kutoa maelezo ya kina kuhusu sababu za kupunguza wafanyakazi.

“Nilielezwa kuhusu zoezi hilo na uchambuzi uliofanyika katika klabu nzima, kwa lengo la kuendelea kukua na kuboresha mambo,” alisema Arteta.

Alion geza: “Baadhi ya maamuzi yanapaswa kufanywa ili kuwaweka watu katika nafasi zinazowafaa na kuendelea kuwekeza ili kufanikisha malengo yetu na mafanikio tunayotarajia kuyajenga. Hilo limeelezwa, lakini kwa hakika mimi si mtu sahihi wa kujibu swali hilo. Natumaini kila mtu atalielewa hilo.”

Baada ya Arteta kuulizwa zaidi kuhusu suala hilo, afisa wa habari wa klabu aliingilia kati na kueleza kuwa suala hilo linapaswa kujibiwa na Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Richard Garlick, badala ya kocha huyo.


SALIBA KUKOSA PICHA

Katika hatua nyingine, Arteta amethibitisha kuwa Arsenal itapiga upya picha rasmi ya kikosi chake kwa msimu wa 2026/27 baada ya beki William Saliba kukosekana kwenye picha ya awali. Klabu hiyo ilieleza kuwa beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa hakuwepo siku ya upigaji picha kutokana na miadi ya kumuona daktari.

Arteta alisema picha hiyo ilikuwa imepangwa kupigwa mara tatu, lakini kila mara ililazimika kuahirishwa dakika za mwisho kwa sababu mbalimbali. Hata hivyo, kutokana na majukumu ya kibiashara ya klabu, waliamua kuendelea na zoezi hilo.

“Kwa hiyo, kilichotokea ni kwamba tulikuwa tumejaribu kupiga picha hiyo mara tatu tayari. Ilibidi tuifute dakika za mwisho kwa sababu tofauti, na tuna majukumu ya kibiashara. Hivyo, tuliamua angalau kupiga picha hiyo,” alisema Arteta, akithibitisha kuwa itarudiwa ili Saliba awepo. Akizungumzia iwapo Saliba alikerwa na kuachwa nje ya picha hiyo, Arteta alisema beki huyo hakuwa na mamlaka ya kuamua kuhusu hali iliyosababisha kukosekana kwake.

“Hilo halikuwa jambo lililokuwa mikononi mwake. Lakini kwa kawaida huwa anafurahia kila kitu. Anajua jinsi anavyopendwa, na watu walikuwa wakimtania kuhusu hilo. Yuko sawa kabisa,”alisema Arteta.