Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CV ya Ibenge yatikisa Misri

IBENGE Pict

Muktasari:

  • Shawky, ambaye aliwahi kuichezea Middlesbrough ya England, amesema amekuwa akimfuatilia Ibenge kwa muda mrefu na kuvutiwa na uwezo wake wa kuongoza timu katika mazingira tofauti ya ushindani.

KOCHA wa ZED FC ya Misri, Mohamed Shawky, amemtaja kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, kuwa mmoja wa makocha bora Afrika, akieleza kuwa uzoefu wake na mafanikio aliyoyapata katika mashindano mbalimbali vimemfanya kuwa miongoni mwa makocha wanaoheshimika katika soka la Afrika.

Shawky, ambaye aliwahi kuichezea Middlesbrough ya England, amesema amekuwa akimfuatilia Ibenge kwa muda mrefu na kuvutiwa na uwezo wake wa kuongoza timu katika mazingira tofauti ya ushindani.

“Namjua kama mmoja wa makocha wazuri Afrika na mwenye uzoefu wa miaka mingi hivyo haitakuwa rahisi kukabiliana naye," amesema kocha huyo ambaye jana usiku, alikuwa na kibarua cha kuiongoza ZED FC dhidi ya Azam katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika.

IBE 01

Ibenge amejijengea jina kubwa katika soka la Afrika kupitia kazi alizofanya katika timu za taifa na klabu mbalimbali, akishiriki mashindano makubwa na kupata mafanikio yaliyompa uzoefu wa kukabiliana na presha ya ushindani wa kimataifa.

Moja ya mafanikio yake makubwa ni kuiongoza DR Congo kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2015, nchini Equatorial Guinea huku 2016, akiiongoza tena DR Congo kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndania (CHAN).

Katika ngazi ya klabu, Ibenge aliweka alama nyingine akiwa na AS Vita Club ya DR Congo, ambayo aliifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2014. Vita Club ilipoteza fainali hiyo dhidi ya ES Sétif ya Algeria kwa sare ya mabao 3-3, lakini ES Sétif ikatwaa ubingwa kwa kanuni ya bao la ugenini.

IBE 02

Baadaye, Ibenge aliendelea na kazi yake katika soka la Morocco akiwa na RS Berkane, klabu aliyoiongoza kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2022 baada ya kuifunga Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa mikwaju ya penalti kwa penalti 5-4, baada ya sare ya bao 1-1.

Uzoefu wake haukuishia DR Congo na Morocco pekee, kwani pia amewahi kufanya kazi Sudan akiwa na Al Hilal kabla ya kuhamia Tanzania na kujiunga na Azam FC ambayo msimu uliopita aliipa rekodi ya kwanza ya kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Huu ni msimu wake wa pili akiwa na Azam na malengo makubwa aliyopewa ni kufika hatua ya makundi lakini kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho la CRDB.