Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagera Sugar kuendeleza moto Ligi Kuu

KAGERA Pict

Muktasari:

  • Kagera inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na morali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City Oktoba 9, 2026 matokeo yaliyoiwezesha kuondoka na pointi tatu muhimu baada ya mwanzo mgumu wa msimu.

KAGERA Sugar inataka kuendeleza ushindi ulioanza kwa kuichapa Mbeya City mabao 3-1, lakini safari hii inakutana na Polisi Tanzania inayohitaji matokeo mazuri ili kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi katika mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba.

Kagera inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na morali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City Oktoba 9, 2026 matokeo yaliyoiwezesha kuondoka na pointi tatu muhimu baada ya mwanzo mgumu wa msimu.

Hata hivyo, changamoto kubwa kwa Kagera itakuwa kuendeleza kiwango hicho mbele ya Polisi Tanzania, ambayo nayo imeonyesha uwezo wa kupata matokeo mazuri tangu ilipopanda daraja mwanzoni mwa msimu.

Katika mechi zake za mwanzo wa msimu wa 2026/27, Kagera ilianza kwa kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Simba, ikatoka sare ya 1-1 na Singida Black Stars, kisha ikafungwa mabao 6-2 na Geita Gold. Baadaye ilipoteza mabao 2-1 dhidi ya Mashujaa na kufungwa 2-0 na Azam kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Fountain Gate.

KAGE 01

Kwa upande wa Polisi Tanzania, timu hiyo ilianza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Azam, ikaifunga JKT Tanzania mabao 2-0 na kuichapa Dodoma Jiji bao 1-0. Hata hivyo, ilipoteza mabao 4-2 dhidi ya Singida Black Stars na baadaye kufungwa 2-1 na Coastal Union.

Kagera itahitaji kutumia vizuri faida ya kucheza nyumbani na kuongeza umakini katika safu yake ya ulinzi. Kufungwa mabao mengi katika baadhi ya michezo ya mwanzo kumeonyesha kuwa timu hiyo inahitaji kupunguza makosa yanayowapa wapinzani nafasi za kufunga.

Kocha wa Kagera Sugar, Cedric Kaze, amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa mchezo huo na kina hamasa ya kuonyesha kile walichokiandaa mazoezini ili kupata matokeo mazuri mbele ya Polisi Tanzania. Kaze anaingia kwenye mchezo huo akiwa na matumaini ya kuendeleza ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City, ambao umeongeza morali kwa wachezaji wake.

KAGE 02

“Tumefanya maandalizi vizuri na tuko tayari kuonyesha uwanjani kile tulichokiandaa kwa ajili ya mashabiki wetu ili kupata matokeo mazuri,” amesema Kaze.

Kwa upande wa Polisi Tanzania, kocha Mbwana Makata aliweka mkazo katika kuongeza umakini wa wachezaji kwa dakika zote za mchezo, hususan katika dakika za mwisho, ili kuepuka kupoteza matokeo.

“Ni muhimu kuwa makini katika dakika zote za mchezo, hasa dakika za mwisho, na kutomdharau mpinzani kwa sababu ligi ina ushindani mkubwa na kila pointi ni muhimu,” ni msisitizo wa benchi la ufundi la Polisi Tanzania.