Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Mexico atumia dakika 24 kuandika rekodi mpya Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Nyota huyo amecheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia na kuweka rekodi hiyo katika ushindi wa kikosi hicho wa mabao 2-0, dhidi ya Afrika ya Kusini.

KIUNGO wa timu ya taifa ya Mexico, Gilberto Mora ameandika rekodi mpya ya kucheza fainali za Kombe la Dunia la mwaka 2026, akiwa na umri mdogo zaidi.

Nyota huyo amecheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia na kuweka rekodi hiyo katika ushindi wa kikosi hicho wa mabao 2-0, dhidi ya Afrika ya Kusini.

Katika mechi hiyo ya ufunguzi ya Kombe la Dunia iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azteca huko Mexico City, Mora alitumia dakika 24, kuandika rekodi baada ya kuingia dakika ya 66, akichukua nafasi ya Alvaro Fidalgo.

Kucheza kwa nyota huyo katika fainali hizi za Kombe la Dunia, kunamfanya awe kijana mdogo zaidi katika historia ya michuano hiyo kwani ana miaka 17 na siku 240.

Pia, Mora anakuwa ni mchezaji mdogo zaidi wa Mexico na kutoka America ya Kaskazini kucheza michuano ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka la Kimataifa la FIFA kwa wanaume.

Mora ni kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Tijuana ya kwao Mexico, ambapo kwa sasa anakuwa mchezaji mdogo zaidi kati ya wachezaji 1,248 walioko kwenye orodha rasmi za timu 48, kwa mujibu wa FIFA.


GILBERTO MORA NI NANI?

Gilberto Rafael Mora Zambrano alikulia Tuxtla Gutierrez, katika jimbo la Chiapas Kusini mwa Mexico, akiwa mtoto wa kiungo wa zamani wa Liga MX. Baba yake, Gilberto Mora Olayo, aliyecheza Toluca, Chiapas, Puebla na Tijuana kabla ya kustaafu mwaka 2011 na kuanza kufundisha.

Olayo ambaye ni Baba yake Mora kwa sasa ni mkufunzi katika mfumo wa vijana wa Klabu ya Tijuana, ambayo pia ndio iliyozalisha kipaji kikubwa cha mwanae.

Mora ana urefu wa futi 5 na inchi 6 (takriban sentimita 168), ni mchezaji mwenye mbinu anayesifika kwa uwezo wake mzuri wa kutengeneza mashambulizi akiwa na jicho kali la pasi.

Katika Kombe la Dhahabu mwaka 2025, kiungo mkongwe, Luis Chavez aliumia na Kocha, Javier Aguirre alimwita Mora mwenye umri wa miaka 16, ambaye alianza nusu fainali dhidi ya Honduras na kutoa asisti ya bao.

 Kiwango bora kwa nyota huyo kimemfanya tishio katika ubunifu katika kikosi cha Tijuana kinachoshiriki Liga MX, akivutia makocha kutoka Real Madrid, Arsenal na Manchester City.

Hata hivyo, moja ya jambo kubwa linalomuumiza mchezaji huyo raia wa Mexico ni sheria ya FIFA inayowazuia wachezaji walio chini ya miaka 18, kuhamia klabu za kigeni.

Mora alicheza mechi yake ya kwanza ya Tijuana Agosti 19, 2024, dhidi ya Santos Laguna akiwa na miaka 15, miezi 10 na siku 5, akiwa ni mchezaji mdogo zaidi kuanza mechi hiyo na mchezaji wa tatu mdogo zaidi kuanza katika historia ya Liga MX.

Siku 12 baadaye, alifunga bao dhidi ya Leon akiwa na umri wa miaka 15 na siku 320, akiwa mchezaji mdogo zaidi kufunga bao katika historia ya Ligi ya juu ya Mexico.

Nyota huyo alicheza mechi yake ya kwanza ya ushindani wa kimataifa akiwa na miaka 16, akianza robo fainali ya Kombe la Dhahabu mwaka 2025, dhidi ya Saudi Arabia.

Wiki mbili baadaye, alianza fainali dhidi ya Marekani, ambapo Mexico iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, na Mora akawa mchezaji mdogo zaidi kushinda mashindano ya kimataifa ya Senior, kulingana na rekodi za Guinness.

Pia, alivunja rekodi zilizokuwa za Lamine Yamal wa Hispania, aliyeshinda Euro 2024 akiwa na miaka 16, na Pele wa Brazil, aliyeshinda Kombe la Dunia mwaka 1958, akiwa na miaka 17.