Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Motlhalo afikisha mechi 100 akiwa na Banyana Banyana

Muktasari:

  • Kiungo huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na pembeni, aliingia kwenye orodha ya wachezaji wachache wa Afrika Kusini waliowahi kufikisha mechi 100 za kimataifa, akiwa mchezaji wa 13 kufanya hivyo.

KIUNGO wa Afrika Kusini, Linda Motlhalo baada ya kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Tanzania ambapo Banyana Banyana ilipoteza kwa mabao 2-1 imemfanya nyota huyo kufikisha idadi ya mechi 100 akiwa na uzi wa timu hiyo.

Kiungo huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na pembeni, aliingia kwenye orodha ya wachezaji wachache wa Afrika Kusini waliowahi kufikisha mechi 100 za kimataifa, akiwa mchezaji wa 13 kufanya hivyo.

Janine van Wyk ndiye anayeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi katika historia ya Banyana Banyana. Beki huyo wa zamani wa Afrika Kusini aliichezea timu ya taifa mara 185, idadi inayomfanya kuwa mchezaji mwenye uzoefu mkubwa zaidi kuwahi kuvaa jezi ya nchi hiyo.

Nyuma yake anafuata Noko Matlou aliyecheza mechi 174, ambaye naye ameacha alama kubwa katika historia ya timu hiyo. Tofauti na Van Wyk aliyekuwa ngome ya ulinzi, Matlou amekuwa tishio zaidi eneo la ushambuliaji, akiwa mmoja wa wafungaji bora wa Afrika Kusini akiweka kambani mabao 66 ya timu ya taifa.

Lakini nyuma ya namba hiyo kuna safari ya mafanikio, changamoto na mchango mkubwa ulioisaidia Afrika Kusini kufanya kuwa moja ya timu zenye ushindani mkubwa barani  Afrika.

Motlhalo alianza kuitumikia timu ya taifa kwa mara ya kwanza Machi 25, 2016, alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Cameroon akianza kwa kufunga bao katika mchezo huo.

Tangu wakati huo amekuwa sehemu muhimu ya timu iliyojenga historia mpya ya Banyana Banyana, kuanzia kushiriki mashindano makubwa hadi kutwaa taji la kwanza la Afrika mwaka 2022.

Katika mechi hizo 100, Motlhalo amekuwa mmoja wa wachezaji wanaoaminika zaidi kuisaidia timu hasa kwenye nyakati za presha.

Katika WAFCON amefunga mabao saba tangu alipoanza kushiriki mwaka 2016, huku sita kati ya hayo yakitokana na penalti.

Uwezo wake wa kubeba majukumu katika mipira ya adhabu ulimfanya kupewa heshima ya kuwa mmoja wa wapigaji bora wa penalti kwenye soka la wanawake Afrika.

Katika timu ya taifa, amefunga mabao 25, akikaribia rekodi za baadhi ya magwiji wa Banyana Banyana waliotangulia.

Akizungumzia hilo Motlhalo alisema “Nimecheza kwenye WAFCON mara nyingi hii ni mara yangu ya tano kushiriki, na nimepata nafasi ya kucheza Kombe la Dunia mara mbili, mwaka 2019 na 2023,”

“Nafasi zipo, fursa zipo, na tutaendelea kufanya kazi kwa bidii. Sote tuna ndoto zetu tuna wachezaji wapya kwenye timu ambao hawajawahi kucheza WAFCON wala kufika Kombe la Dunia,† alisema Motlhalo akieleza sababu inayomfanya aendelee kuthamini kile ambacho soka limempa katika maisha yake

Kocha wa Banyana Banyana, Desiree Ellis alisema kiungo huyo amekuwa moja ya wachezaji muhimu kikosini akiwa na uwezo wa kubadilisha mchezo.

“Kila anapoingia uwanjani anakufanya ubaki ukimwangalia. Anafunga mabao muhimu katika nyakati muhimu,† alisema Ellis.