Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nicolas Batum asema inatosha!

Muktasari:

  • Batum mwenye umri wa miaka 37, ametangaza kustaafu kwake kupitia video aliyoweka kwenye mitandao ya kijamii akiwa pamoja na mwanawe.

LOS ANGELES, MAREKANI: MCHEZAJI wa nafasi mbalimbali katika mchezo wa kikapu, Nicolas Batum ameamua kustaafu baada ya kucheza kwa miaka 18 katika Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) pamoja na kipindi kirefu akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa.

Batum mwenye umri wa miaka 37, ametangaza kustaafu kwake kupitia video aliyoweka kwenye mitandao ya kijamii akiwa pamoja na mwanawe.

“Nimeamua kustaafu kucheza mpira wa kikapu kwa sababu kadhaa,” Batum alimwambia mwanawe mwenye umri wa miaka 10, Ayden, katika video hiyo.

“Nataka kurudi nyumbani na kuwa pamoja nawe. Nitakutunza na kutoa nafasi kwa wengine. Nafikiri muda wangu umefika mwisho. Muda wangu na Ufaransa uliisha miaka miwili iliyopita. Na NBA pia imekwisha. Unajua, unapokuwa umecheza mpira wa kikapu kwa muda mrefu kama mimi, wakati fulani lazima ujue ni lini wa kustaafu. Nimefanya kila nilichohitaji kufanya.”

Batum alicheza misimu miwili katika ligi ya Ufaransa kabla ya kuchaguliwa katika raundi ya kwanza ya mchujo wa NBA na Portland Trail Blazers. Mchezaji huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 7 alitumia misimu saba Portland kabla ya kucheza misimu sita iliyofuata akiwa Charlotte.

Batum alitumia sehemu kubwa ya misimu yake sita ya mwisho akiwa Los Angeles Clippers, huku akiwa na kipindi kifupi Philadelphia 2023/24.  Pia alikuwa mchezaji muhimu katika timu za taifa za Ufaransa zilizoshinda medali za fedha katika Michezo ya Olimpiki 2020 na 2024.

Batum alimalizia maisha yake ya NBA akiwa na wastani wa pointi 9.6, ribaundi 4.7 na asisti 3.0 kwa mchezo, huku akitupia kwa asilimia 37 kutoka umbali wa pointi tatu.