Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Newcastle yamjibu Isak, mambo yazidi kutibuka

Muktasari:

  • Mchezaji huyo anayetaka kuondoka alilalama kwamba “uaminifu umepotea” kati yake na klabu ambayo anadai imekiuka makubaliano yao.

NEWCASTLE, ENGLAND: NEWCASTLE United imemjibu mshambuliaji wao wa kimataifa wa Sweden, Alexander Isak baada ya staa huyo kutoa tamko zito kupitia mitandao ya kijamii.

Mchezaji huyo anayetaka kuondoka alilalama kwamba “uaminifu umepotea” kati yake na klabu ambayo anadai imekiuka makubaliano yao.

Hata hivyo, uongozi wa Newcastle umeweka wazi kuwa Isak hakuambiwa wakati wowote kwamba anaweza kuondoka katika majira haya ya kiangazi na kwa mshangao, wamemwambia kwamba yupo huru kurejea kikosini.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliondolewa kwenye kikosi cha kwanza cha Newcastle baada ya kulazimisha kuondoka katika majira haya ya kiangazi kwenda Liverpool.

Isak hakuwepo katika kambi ya mazoezi ya maandalizi ya msimu iliyojifua huko Asia.

Baada ya sintofahamu ya muda mrefu sasa  kwa mara ya kwanza, ameweka wazi msimamo wake hadharani akisema kuwa “itakuwa kwa manufaa ya kila mtu” kama ataondoka.

Isak aliandika:"Najivunia kutambuliwa na wachezaji wenzangu kwa kuingia kwenye kikosi bora cha PFA cha Ligi Kuu kwa msimu wa 2024-25.

Kwanza kabisa, nataka kuwashukuru wachezaji wenzangu na kila mmoja katika klabu ya Newcastle United."

"Sipo kwenye hafla hii (Hafla ya tuzo za PFA usiku wa jana) leo. Kwa hali ilivyo sasa, sikuhisi kama ni sahihi kuwepo. Nimekaa kimya kwa muda mrefu wakati wengine wakizungumza. Ukimya wangu umewaruhusu watu kunizushia mambo ambayo wanajua sio kile kilichokubaliwa hapo awali."

"Ukweli ni kwamba ahadi ilitolewa hapo awali na klabu, hivyo wanajua  msimamo wangu kwa muda mrefu. Sasa kuonekana kwamba haya masuala ndiyo yanaibuka hivi karibuni ni upotoshaji.

"Ahadi zikivunjwa na uaminifu ukipotea, uhusiano hauwezi kuendelea. Hali hiyo ndio niliyo nayo kwa sasa na ndiyo maana mabadiliko yanahitajika kwa ajili ya manufaa ya kila mtu, si mimi pekee."

Baada ya kauli hiyo saa chache baadaye, Newcastle wakatoa tamko lao wakisema hawatamuuza Isak isipokuwa watakapoona kuna maslahi ya klabu.

Taarifa yao ilisema:"Tunavunjika moyo kuona ujumbe wa mitandao ya kijamii kutoka kwa Alexander Isak usiku huu. Tunataka kuweka wazi kwamba Alex bado yuko chini ya mkataba na hakuna kiongozi wa klabu aliyewahi kutoa ahadi kwamba anaweza kuondoka Newcastle United katika dirisha hili. Tunataka kubaki na wachezaji wetu bora, lakini pia tunafahamu wachezaji wana matakwa yao na tunasikiliza maoni yao.

Kama tulivyoeleza kwa Alex na wawakilishi wake, kila uamuzi lazima uangalie maslahi ya Newcastle United, timu na mashabiki wetu. Tumekuwa wazi kwamba masharti ya mauzo majira haya hayajafikiwa na hatuoni yakifikiwa."

"Hii ni klabu yenye fahari na historia kubwa, na tunajitahidi kudumisha hisia za kifamilia. Alex bado ni sehemu ya familia yetu na atakaribishwa kurejea pindi atakapokuwa tayari kuungana na wenzake.”

Inafahamika kwamba msimamo mkali wa Isak unatokana na ahadi ya nyongeza ya mshahara iliyoahidiwa na wamiliki wa zamani, Amanda Staveley na Mehrdad Ghodoussi ambayo haijatekelezwa.

Mkurugenzi wa michezo wa zamani, Paul Mitchell, alikuwa ameahirisha mazungumzo hayo kwa sababu Isak bado ana mkataba wa miaka minne na analipwa Pauni 130,000 kwa wiki.

Hata baada ya Mitchell kuondoka, Newcastle kuwa tayari kuvunja ukomo wao  wa juu ya mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki ili kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu, uhusiano kati ya Isak na Newcastle unaonekana kuvunjika kabisa.

Lakini jibu la Newcastle kwa ujumbe wa Isak linaonyesha kwamba wanakanusha kumwahidi chochote staa huyo.

Kwa mujibu wa SunSport, Liverpool wameidhinisha dau la Pauni 130 milioni kwa ajili ya kumsajili Isak na linaweza kuwasilishwa katika siku chache zijazo.

Iwapo ofa hiyo itakubaliwa, matumizi ya Liverpool kwenye usajili katika dirisha hili yatapanda hadi kufikia Pauni 400 milioni.

Awali mwezi huu, Liverpool ilikataliwa ofa ya Pauni 110 milioni ambayo iliwasilisha kwa ajili ya Isak.