Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NBA yazindua mwonekano mpya wa viwanja 2026/27

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa NBA, viwanja hivyo vyenye miundo ya kuvutia vitatumika katika hatua ya makundi, robo fainali na nusu fainali vikilenga kuleta mwonekano wa kipekee na unaofanana katika michezo yote ya Emirates NBA Cup.

WASHINGTON, MAREKANI: SHIRIKISHO la Kikapu Marekani (NBA), limezindua miundo hiyo kupitia video na picha, ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya mwaka huu yatakayoanza Ijumaa, Oktoba 30. Mechi mbili zitafungua mashindano hayo; New York Knicks itamenyana na Philadelphia 76ers katika mchezo wa kwanza, kabla ya Los Angeles Lakers kukutana na Golden State Warriors katika mchezo wa pili.

Kwa mujibu wa NBA, viwanja hivyo vyenye miundo ya kuvutia vitatumika katika hatua ya makundi, robo fainali na nusu fainali vikilenga kuleta mwonekano wa kipekee na unaofanana katika michezo yote ya Emirates NBA Cup.

Muundo wa viwanja vya mwaka huu unapambwa na kampeni ya Nike inayoitwa “End of Ordinary”, ikiwemo maandishi makubwa ya majina ya timu yaliyotokana na koti maalumu la mchezo lililomo katika mkusanyiko huo wa mavazi. Pia, viwanja hivyo vimeboreshwa ili rangi na mwonekano wake vitofautiane na jezi za nyumbani za timu.

Kaulimbiu ya mashindano ya msimu ujao “Timu 30. Nane zitasonga mbele. Bingwa mmoja,” itaonekana karibu na mstari wa alama tatu katika kona za viwanja hivyo.

TIMU 30, MAKUNDI SITA

Timu zote 30 zimegawanywa katika makundi sita, kila moja likiwa na timu tano. Michezo ya hatua ya makundi itachezwa Ijumaa kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 27, katika siku ambazo NBA imezipa jina la Cup Nights. Baada ya hatua hiyo, timu nane zitafuzu kwa hatua ya mtoano, huku  robo na nusu fainali zikichezwa katika viwanja vya nyumbani vya timu husika.

Timu mbili zitakazofanikiwa kufika fainali zitachuana Desemba 11 katika uwanja wa Hinkle Fieldhouse, uliopo Indianapolis, Marekani.

Mashindano ya mwaka huu yatakuwa ya nne ya NBA Cup tangu kuanzishwa kwa mfumo huo wa mashindano ya katikati ya msimu.

Los Angeles Lakers ilitwaa taji la kwanza katika msimu wa 2023-24, Milwaukee Bucks ikashinda lililofuata kabla ya New York Knicks kutwaa ubingwa wa msimu uliopita na kuingia kwenye mashindano ya mwaka huu ikiwa bingwa mtetezi.

Katika fainali mwaka jana, Knicks iliifunga San Antonio Spurs. Kwa namna ya kipekee, mchezo huo ulionekana kama utangulizi wa kile kilichoweza kuwa pambano la Fainali za NBA, na baadaye New York ikaendeleza ubora wake kwa kuibuka na ushindi katika mfululizo wa michezo mitano dhidi ya Victor Wembanyama na wenzake.