Wembanyama apiga tizi na timu ya raga Ufaransa
Muktasari:
- Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye ana urefu wa futi 7 na inchi 4 (takribani sentimita 224) na uzito wa takribani kilo 107, anafahamika kwa kutafuta njia mbalimbali zisizo za kawaida za kuboresha uwezo wake uwanjani. Mwaka 2025, Wembanyama alitumia wiki mbili nchini China akijikita katika kuimarisha nguvu za mwili na akili akiwa pamoja na watawa wa Shaolin.
PARIS, UFARANSA: WAKATI Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) msimu wa 2026/27 ikitarajiwa kuanza Oktoba 20, 2026, supastaa Victor Wembanyama amesema alivutiwa na umoja na mshikamano uliopo katika mchezo wa raga baada ya kutumia sehemu ya mapumziko akifanya mazoezi na Klabu ya Provence, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Ufaransa.
Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye ana urefu wa futi 7 na inchi 4 (takribani sentimita 224) na uzito wa takribani kilo 107, anafahamika kwa kutafuta njia mbalimbali zisizo za kawaida za kuboresha uwezo wake uwanjani. Mwaka 2025, Wembanyama alitumia wiki mbili nchini China akijikita katika kuimarisha nguvu za mwili na akili akiwa pamoja na watawa wa Shaolin.
Katika safari yake ya hivi karibuni, Wembanyama alionekana akifanya mazoezi ya kugonga pedi za rugby kwa mtindo wa tackle, akishiriki mazoezi ya kupokezana mipira, akifanya mazoezi ya line-out, pamoja na kusimama kwa urefu mkubwa kuliko wachezaji wenzake wakati timu ya Provence ilipokuwa kwenye kikao cha pamoja kabla ya mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu mwezi Agosti.
Pia alirekodiwa akikumbatiana kwenye chumba cha kubadilishia nguo na Teimana Harrison, aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya England na kupata mechi tano za kimataifa mwaka 2016, na ambaye sasa anachezea Provence.
"It was a great experience, seeing the team spirit they have over there," alisema Wembanyama, ambaye katika safari hiyo aliambatana na mchezaji mwenzake wa San Antonio Spurs, Harrison Barnes.
Alisema uzoefu huo ulimvutia hasa kutokana na uhusiano uliopo kati ya wachezaji, makocha na mashabiki.
"Ilinitia moyo sana kuona uhusiano uliopo kati ya wachezaji wenzangu, makocha na mashabiki. Mazoezi yalikuwa magumu sana, lakini pia yalikuwa mazuri kwa ajili ya kuimarisha uimara wa mwili, namna ya kusogea na kujenga nguvu.
"Lakini ninachoshukuru zaidi ni namna nilivyopokelewa. Sijawahi kupokelewa mahali popote kwa namna hii. Sikuwa sehemu ya timu, lakini walinichukulia kana kwamba nilikuwa sehemu yao. Ningependa kufanya hivi tena."
Wembanyama aendelea na shughuli nyingine
Wembanyama aliunganisha mazoezi yake na Provence na kuandaa tukio lake la Hoop Gambit katika mji alikozaliwa wa Le Chesnay.
Katika tukio hilo, washiriki hucheza michezo ya chess na basketball, wakichanganya mchezo wa akili na mchezo wa mpira wa kikapu.
Timu yake ya San Antonio Spurs ilikaribia kutwaa ubingwa wa NBA mapema mwaka huu, lakini ilifungwa kwa jumla ya michezo 4-1 na New York Knicks mwezi Juni.
Kwa upande wa Provence, klabu hiyo ambayo hapo awali imewahi kuwa na wachezaji wa kimataifa wa Wales kama George North na Tomas Francis, imeanza vizuri msimu wake na kampeni ya kutafuta kupanda daraja hadi Top 14, ligi ya juu kabisa ya rugby nchini Ufaransa.
Provence imeshinda mechi zake tano za kwanza za ligi.