Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gallagher atajwa mbioni kutua Old Trafford

Muktasari:

  • Inaelezwa Man United inapendelea kumsajili kwa mkopo dirisha la usajili la Januari, lakini itaweka kipengele cha kumnunua mazima mwisho wa msimu ikiwa itaridhishwa na kiwango chake.

BENCHI la ufundi la Manchester United limeorodhesha majina ya viungo saba wanaowafuatilia kwa ajili ya kuimarisha safu ya kiungo na staa wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya England, Conor Gallagher, 25, ni miongoni mwa machaguo yao.

Inaelezwa Man United inapendelea kumsajili kwa mkopo dirisha la usajili la Januari, lakini itaweka kipengele cha kumnunua mazima mwisho wa msimu ikiwa itaridhishwa na kiwango chake.

Gallagher, aliyewahi kucheza Chelsea, hivi karibuni amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha Diego Simeone, jambo linalomfanya ahitaji kuondoka ili kupata timu itakayompa nafasi ya kucheza na kujiwekea asilimia nyingi za kuitwa kikosi cha England kitakachoshiriki Kombe la Dunia.

Kiungo huyu anajulikana kwa uwezo wake wa kukaba, kasi na kupandisha mashambulizi, jambo ambalo linamvutia sana kocha Ruben Amorim.

Mkataba wake Atletico Madrid unamalizika hadi mwaka 2028 na hadi sasa bado hakuna majibu kamili ikiwa timu hiyo itakuwa tayari kumwachia au itamweka ngumu.

Antoine Semenyo

ASTON Villa imeanza mawasiliano na mawakala wa winga wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Wales, Brennan Johnson, 24, ambaye kwa sasa haonekani kuwa  kwenye mipango ya kocha Thomas Frank. Johnson amekuwa akipata dakika chache za kucheza Tottenham msimu huu, hali iliyofungua mlango kwa klabu nyingine kuonyesha nia ya kumsajili. Mbali ya Aston Villa, Crystal Palace pia inataka kumsajili.

Joshua Zirkzee

ROMA imewasilisha ofa ya Euro 5 milioni kwenda Manchester United ili kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Joshua Zirkzee, 24, dirisha la Januari kwa mkopo wa mwaka mmoja. Kwa mujibu wa taarifa, Roma pia wameweka kipengele cha kuongeza Euro 30 milioni 30 ifikapo Juni ili kuufanya usajili huo kuwa wa kudumu. Zirkzee amekuwa hapati nafasi ya kutosha kwenye viunga vya Old Trafford.

Jeremy Monga

CHELSEA na Manchester City zinaonyesha nia ya kumsajili winga wa timu za vijana za England, Jeremy Monga, 16, anayekipiga katika klabu ya Leicester City inayoshiriki Ligi ya Daraja la kwanza England. Nyota huyo chipukizi amevutia vigogo hao kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha licha ya umri wake. Inaelezwa vigogo hao wanaweza kujaribu kumsajili dirisha la Januari na ikishindikana watasubiri hadi mwisho wa msimu.

Brennan Johnson

ASTON Villa imeanza mawasiliano na mawakala wa winga wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Wales, Brennan Johnson, 24, ambaye kwa sasa haonekani kuwa  kwenye mipango ya kocha Thomas Frank. Johnson amekuwa akipata dakika chache za kucheza Tottenham msimu huu, hali iliyofungua mlango kwa klabu nyingine kuonyesha nia ya kumsajili. Mbali ya Aston Villa, Crystal Palace pia inataka kumsajili.

Joshua Zirkzee

ROMA imewasilisha ofa ya Euro 5 milioni kwenda Manchester United ili kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Joshua Zirkzee, 24, dirisha la Januari kwa mkopo wa mwaka mmoja. Kwa mujibu wa taarifa, Roma pia wameweka kipengele cha kuongeza Euro 30 milioni 30 ifikapo Juni ili kuufanya usajili huo kuwa wa kudumu. Zirkzee amekuwa hapati nafasi ya kutosha kwenye viunga vya Old Trafford.

William Osula

NEWCASTLE United inaendelea kufanya mazungumzo na Eintracht Frankfurt inayohitaji kumsajili mshambuliaji wao William Osula, 22, kwa mkopo wa nusu msimu. Osula, ambaye ana asili ya Denmark licha ya kucheza timu za vijana za Ujerumani, anatamani sana kucheza Bundesliga baada ya kuona nafasi yake katika kikosi cha Newcastle ni finyu. Mchezaji huyo kwa sasa anasubiri klabu hizo mbili kufikia makubaliano.

Ruben Neves

Newcastle United imeingia vitani na Manchester United kuipata saini ya kiungo wa Ureno, Ruben Neves, 28, anayeichezea Al-Hilal. Ripoti zinaeleza klabu yake ya sasa Al-Hilal ya Saudi Arabia iko tayari kumuuza dirisha la Januari, jambo linaloongeza uwezekano wa kurejea kwake barani Ulaya. Neves ana uzoefu mkubwa wa Ligi Kuu England alioupata akiwa na Wolves.

Endrick

REAL Madrid imekubali kumtoa mshambuliaji wao chipukizi, Endrick, 19, kwa mkopo wa miezi sita kwenda Olympique Lyon ya Ufaransa. Uamuzi huo umefanywa ili kumpa Endrick nafasi zaidi ya kucheza na kuzoea soka la Ulaya baada ya kuonekana hana nafasi katika kikosi cha Madrid. Lyon wanaamini ujio wa Endrick utaongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji kwa nusu ya pili ya msimu.