Namba za Fermin Lopez hazijawahi kudanganya
Muktasari:
- 4- NA akiwa na umri wa miaka 21 na siku 260, Fermin Lopez ndiye mchezaji mdogo zaidi wa Barcelona kuwahi kuhusika na mabao manne katika mechi moja ya LaLiga (mabao mawili, asisti mbili), tangu Bojan Krkic dhidi ya Real Valladolid Machi 2008 (miaka 17 na siku 208).
2+2- FERMIN Lopez ndiye mchezaji wa kwanza wa Barcelona kufunga mabao mawili na kutoa asisti mbili za mabao katika mechi ya LaLiga tangu Lionel Messi alivyofanya hivyo mwezi Oktoba 2019 dhidi ya Real Valladolid.
4- NA akiwa na umri wa miaka 21 na siku 260, Fermin Lopez ndiye mchezaji mdogo zaidi wa Barcelona kuwahi kuhusika na mabao manne katika mechi moja ya LaLiga (mabao mawili, asisti mbili), tangu Bojan Krkic dhidi ya Real Valladolid Machi 2008 (miaka 17 na siku 208).
3 - NA katika umri wa miaka 21 na siku 260, Fermín López ndiye mchezaji mdogo zaidi wa Barca kuhusika katika mabao matatu katika mechi moja ya LaLiga (mabao mawili, asisti moja) tangu Ansu Fati dhidi ya Real Sociedad mnamo Agosti 2022 (miaka 19 na siku 294; bao moja, asisti mbili). Hata hivyo kahusika nayo manne dhidi ya Valencia.
1 - FERMIN Lopez amefunga na kutoa asisti katika mechi moja kwa mara ya kwanza akiwa na timu ya wakubwa ya Barcelona kwenye mashindano yote baada ya mechi 63.
7- VALENCIA wamefungwa mabao saba au zaidi katika mechi moja ya LaLiga kwa mara ya nane katika historia, na juzi (vs Barcelona) ilikuwa ni mara ya kwanza tangu Machi 1955 walipocheza dhidi ya Alaves (7-0).
5 - BARCELONA wamefunga mabao matano katika kipindi cha kwanza cha mechi ya LaLiga kwa mara ya kwanza tangu Aprili 2015 dhidi ya Getafe wakiwa chini ya kocha Luis Enrique Martínez.
100 - BARCELONA wamefunga mabao 100 katika mechi 32 tu kwenye mashindano yote chini ya Hans-Dieter Flick, na kumfanya kuwa kocha wa pili kufikia idadi hiyo kwa haraka akiwa na Barça baada ya Helenio Herrera 1959 (mechi 31).
3 - BARCELONA wamefunga mabao matatu ndani ya dakika 15 za kwanza mechi ya LaLiga kwa mara ya tatu katika karne ya 21, baada ya kufanya hivyo Aprili 2008 dhidi ya Valencia na Oktoba 2008 dhidi ya Atletico Madrid.