Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzigo mpya EPL, mambo mapya

MZIGO Pict

Muktasari:

  • Kwa usiku huo mabingwa watetezi Liverpool walikuwa na kibarua kizito uwanjani Anfield kumenyana na Bournemouth.

LONDON, ENGLAND: MSIMU wa 2024-25 ukiwa umemalizika muda si mrefu, tayari mchakamchaka mpya wa 2025-26 wa Ligi Kuu England umeanza rasmi usiku wa jana Ijumaa.

Kwa usiku huo mabingwa watetezi Liverpool walikuwa na kibarua kizito uwanjani Anfield kumenyana na Bournemouth.

Kwenye Ligi Kuu England msimu huu kutakuwa na mabadiliko kibao, yasiyopungua 13 ikiwamo sheria na kanuni mpya kabisa ambazo mashabiki walikuwa hawazifahamu, kwa sababu zilikuwa haziwahi kutumika.

Badiliko la kwanza ni kwamba mpira utakaotumika si wa Nike tena. Hiyo ni baada ya Ligi Kuu England kusitisha miaka 25 ya ushirika na kampuni ya Nike, ambapo mpira wa Ligi Kuu England utakaotumika msimu huu utatengenezwa na Puma.

Na mpira wa kwanza wa Pume kwenye Ligi Kuu England uliotengenezwa na kampuni hiyo ya Ujerumani utafahamika kwa jina la Orbita Ultimate PL.

Lakini, ni kitu gani kingine kitakuwa tofauti msimu huu?

MZI 01

Kanuni mpya

Katika kutekeleza sheria zinazoongoza mchezo wa soka, kwenye Ligi Kuu England wanajaribu kuondoa kasoro zote ambazo zimekuwa zikileta shida. Kwenye Ligi Kuu England msimu huu kutakuwa na njia mbadala ya timu kupewa pigo la mpira wa kona.

-Kibano cha kupoteza muda, ambako makipa wenye kawaida ya kupoteza muda, msimu huu waamuzi wataanza kuhesabu sekunde tano tu na kama kipa atashindwa kuanzisha mpira, zikifika sekunde nane tu mpinzani anapewa faida ya kupiga pigo la mpira wa kona.

-Usikumbatie ndani ya boksi, ambapo waamuzi sasa wamepewa ruhusa ya kutoa adhabu kwa mchezaji anayemkumbatia mwenzake ndani ya boksi ili kukomesha kawaida ya wachezaji kushikana na kuangushana kama mieleka.

-Kibao kwa wachezaji wenye kawaida ya kujiangusha na wanaodanyanya na hilo adhabu yake itakwenda hadi kwa makocha kama si klabu kwa ujumla.

-Ligi Kuu England imekubaliana pia ni manahodha tu wa mchezo ndiyo watakaoruhusiwa kuzungumza na mwamuzi inapokuwa na tatizo na si kuruhusu wachezaji wengine kumzonga refa wa mchezo pindi wanapohisi uamuzi umekwenda kinyume dhidi yao.

-Mchezaji hataoonyeshwa kadi nyingine ya njano endapo atakuwa amekasirika kufuatia tukio la kuonyeshwa kadi ya njano ya kwanza baada ya kufanya faulo.

MZI 03

Mabadiliko mengine

Kwenye Ligi Kuu England msimu huu mechi nyingi zitarushwa mubashara, ambapo Sky Sports, itarusha walau mechi 215 na TNT itarusha 52.

Waamuzi pia watachezesha huku wakiwa wamevaa kamera, ambapo hilo litaanza kutumika kwenye wikiendi ya tatu ya msimu huu ili kuwapa mashabiki fursa ya kuona matukio ya karibu zaidi yanayotokea uwanjani.

Dili mpya za televisheni zitaruhusiwa pia kwenye vyumba vya kubadilishia na kufanya mahojiano na makocha na wachezaji wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza. Kutakuwa na michoro mingi zaidi ya ndani ya uwanja kuhusu VAR ili kuonyesha matukio ya kuotea na waamuzi watakuwa na kazi ya kuwaeleza mashabiki wanapofanya mabadiliko ya uamuzi wao.

MZI 02

Viwanja vipya

Hatimaye kutakuwa na viwanja vipya vitakavyotumika kwenye Ligi Kuu England msimu huu, hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa miaka ya karibuni.

Elland Road, Turf Moor na Stadium of Light, viwanja vya nyumbani vya timu tatu zilizopanda msimu huu vitatumika kwenye Ligi Kuu England baada ya muda mrefu. Lakini, Uwanja wa Hill Dickinson haujawahi kutumika.

Uwanja huo utatumiwa na Everton msimu huu, ambapo uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 52,769 utakuwa wa 62 kutumika kwenye zama za Ligi Kuu England. Everton haitatumia uwanja wake wa Goodison Park msimu huu, ambao ilianza kuutumia tangu 1892.