Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mstaafu Fury aachia video ikiacha utata

FURY Pict

Muktasari:

  • ‘The Gypsy King’ alitangaza kustaafu Januari, mwaka huu, baada ya kupoteza mapambano mfululizo dhidi ya Oleksandr Usyk.

LONDON, ENGLAND: TYSON Fury bado anaendelea kuweka mwili wake fiti huku mashabiki wa ngumi wakisubiri kwa hamu kurejea kwake ulingoni.

‘The Gypsy King’ alitangaza kustaafu Januari, mwaka huu, baada ya kupoteza mapambano mfululizo dhidi ya Oleksandr Usyk.

Hata hivyo, katika wiki za hivi karibuni, Fury ameashiria kuwa anaweza kubadili uamuzi huo na kurudi tena kupigana.

Mara ya kwanza alizua tetesi za kurejea baada ya kuweka video akiwa gym na kocha wake wa muda mrefu, SugarHill Steward mwezi uliopita.

F 01

Katika video hiyo Fury anasema: “Nipo gym. Nimekutana na mtu ambaye mnampaswa kumjua,” kabla ya kuelekeza kamera kwa Steward. Kisha, akaongeza: “Mnajua kinachokuja...” na papo hapo Steward akajibu: “Mnajua ni wakati gani huu.”

Sparring ni mazoezi ya kupigana kati ya mabondia wawili kwa lengo la kujifunza, kuongeza uzoefu na au kujiandaa kwa pambano halisi bila dhamira ya kumuumiza mpinzani kwa makusudi.

F 02

Tangu hapo, Fury hajaacha kufanya mazoezi, bali ameongeza kasi na mapema wiki hii alifanya 'sparring' ya raundi 12 dhidi ya bondia asiye na rekodi ya kupoteza Ricky Gorman, na aliweka video akifanya mazoezi na begi la maji (aqua bag), akionekana mwepesi na mwenye kasi.

Baada ya video hizo mashabiki walianza kumiminika kutoa maoni, ambapo mmoja aliandika: “Anaonekana kuwa na nguvu zaidi.”, huku mwingine akiandika, “wakati wowote, mahali popote. Uingereza mara ijayo watu 100,000.”, ilhali mwingine aliongeza: “Anarudi akiwa bora zaidi kuliko mwanzo.” na mwingine alidai: “Anacheza kama bingwa wa uzito wa kati.”

F 03

Wakati mashabiki wakisubiri pambano la muda mrefu la Waingereza wawili — kati ya Fury na Anthony Joshua — Fury ameeleza kuwa kwa sasa anavutiwa zaidi na pambano dhidi ya Usyk na hivi karibuni alimwandikia mpinzani wake huyo ujumbe wa moja kwa moja kwenye Instagram, akisema: “Mpige mara mbili, dunia inajua ukweli.”

Meneja wake, Spencer Brown naye aliliambia Boxing News kuwa pambano la tatu dhidi ya Usyk ndilo linaloweza kumfanya Fury arudi tena ulingoni.

“Ameshatangaza kustaafu, lakini huwezi kujua. Yeye ni mtu wa ajabu sana. Bila yeye, mchezo hauna ladha kama zamani. Kwa sasa anafurahia maisha, ana mambo mengi ya kufanya," alisema.

F 04

Lakini akiamua na akiridhika, huenda akarejea. Na kama mkwanja utakaowekwa mezani kwenye pambano hilo utakuwa mkubwa, maana yake ni kwamba atakuwa na hesabu kali na nzito za kurejea.

"Lakini nadhani atarudi kwa ajili ya Usyk. Itabidi alipwe fedha nyingi kwa ajili ya pambano hilo, lakini nadhani atakubali,” alisema.