Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hispania bingwa wa dunia, Argentina ikiteseka 

BINGWA Pict

Muktasari:

  • Bao la dakika ya 106 likifungwa na mshambuliaji Ferran Torres kwa mguu wa kushoto akipokea pasi ya kichwa ya Nico Williams, likatosha kuamua mchezo huo.

Hispania imefanikiwa kubeba Kombe la Dunia mwaka 2026 baada ya kuivua ubingwa huo Argentina kwa ushindi wa  bao 1-0.

Bao la dakika ya 106 likifungwa na mshambuliaji Ferran Torres kwa mguu wa kushoto akipokea pasi ya kichwa ya Nico Williams, likatosha kuamua mchezo huo.

Dakika 90 za mchezo huo zilikamilika huku timu zote zikiwa hazijafungana lakini Hispania ndio imekuwa na mchezo mzuri ikitawala vyema mwanzo mwisho.

Hispania ikatengeneza mashambulizi 16 yaliyolenga lango na katika hayo 11 yakaokolewa kiufundi na kipa Emiliano Martinez akiibeba nchi yake kwa kazi nzuri.

Argentina haikuwa na makali kwenye mchezo huo katika safu yake ya ushambuliaji ikicheza dakika 120 bila kuwa na shuti lililolenga lango ambapo mashuti yake mawili yalitoka nje.

Takwimu nyingi zilikuwa bora kwa Hispania, ilitawala mchezo kwa asilimia 65 dhidi ya 35, huku ikutengeneza nafasi nne za wazi za kufunga wakati Argentina haikufanikiwa hata moja. Hii ilionesha namna Argentina ilivyoteseka.

Hispania ndio ikawa ya kwanza kutengeneza shambulizi zuri dakika ya nne, shuti la Kiungo Lamine Yamal likaishia kuwagonga mabeki wa Argentina, kisha kipa Emiliano Martinez akawahi na kudaka.

Argentina nayo ikatengeneza nafasi nzuri dakika ya sita, kipa wa Hispania, Unai Simon akawahi kutoka akimdhibiti Lionel Messi aliyekuwa anataka kwenda kufunga.

Mshambuliaji Mikel Oyarzabal dakika ya 38 alipata nafasi nzuri nje kidogo ya eneo la hatari lakini shuti lake kali likadakwa vizuri na Martinez.

Licha ya Argentina kupata pigo kipindi cha kwanza ikiwapoteza mabeki wake wawili wa kati, Lisandro Martinez na Christian Romero kwa maumivu, lakini bado kikosi chao kikaonyesha ubora wa kujua kucheza kwa nidhamu bora ya kuzuia.

Argentina ikapata pigo lingine dakika ya 90+3 kwa kiungo wake Enzo Fernandez kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuzaa nyekundu, baada ya kupata kadi mbili za njano ndani ya dakika 11 za muda wa dakika 90.

Hilo linakuwa taji la pili kwa Hispania la Kombe la Dunia ambapo mara ya kwanza ililichukua mwaka 2010 kwenye fainali zilizofanyika nchini Afrika Kusini ambako nako ililichukua kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uholanzi.